Vocal Africa yaelekea Mahakamani Kenya kutaka Twaha Mwaipaya afichuliwe alipo

Vocal Africa yaelekea Mahakamani Kenya kutaka Twaha Mwaipaya afichuliwe alipo

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314

​
Siku tatu tangu Mwanaharakati Mtanzania Twaha Mwaipaya aripotiwe kutekwa katika eneo la Kamulu, Kenya, hatua mpya imechukuliwa kutaka mamlaka zieleze alipo.

Shirika la Vocal Africa leo linawasilisha ombi la kisheria la habeas corpus katika Mahakama za Milimani likilenga kumtaka Twaha afikishwe mahakamani na mamlaka zinazohusika zieleze alipo.

Miongoni mwa walioorodheshwa kama walalamikiwa ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Ruai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hatua hii inakuja wakati mashirika ya haki za binadamu yakizitaka mamlaka za Kenya kuhakikisha usalama wa Twaha na kuchunguza mazingira ya kupotezwa kwake.

1793275025138.png

Kwa Kenya, suala hili linaibua maswali mazito kuhusu wajibu wa Serikali kulinda watu walio ndani ya mipaka yake, wakiwemo raia wa nchi jirani wanaoishi nchini.


Je, hatua ya kwenda mahakamani ndiyo njia muhimu zaidi sasa ya kupata majibu kuhusu alipo Twaha au mamlaka za Kenya zinapaswa kutoa maelezo ya wazi mara moja bila kusubiri shinikizo la mahakama?
 

Attachments

  • 2765.jpg
    2765.jpg
    240.7 KB · Views: 11
Back
Top Bottom