Vodacom acheni wizi wa waziwazi

Mkuu mimi voda kifurushi cha mwez wananipa gb7 na sio 10 na zina kata balaaa narudi zangu tiGo.
Tigo na Voda ni mtu na Binamu yake. Nilipohangaika sana na hii mitandao nilihamia Airtel sikuipenda ilikuwa slow sana, kisha nikaenda Halotel nikapata furaha kwa mda flani wakatubadilikia napo...nilopojaribu Zantel nilipata pumziko la nafsi sasa. Naelekea mwaka wa 3 sasa offer hazibadiliki hovyo na vifurushi vinauzwa kwa uaminifu. Havichakachuliwi yani sio unauziwa 1GB ya kiini macho kumbe umepewa 500MB kwa uhalisia.

To prove that, tunaweza play content kwa youtube wote tukiwa na 1GB ila utashangaa ww MB zimekata mimi zangu bado zipo.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!!! Nina uhakika huwez angalia movie ukaimaliza kwa 1GB ila mie namaliza bila stress.
 
Yani hawa voda wanaendelea kuwatesa sababu mnawaendekeza sana pamoja na upuuzi wao wote.....hivi kwa kuhama ni mpaka ukate viza ubalozi wa china nyie mbwehaaa!!??
 
Dah! MAmbo ndo hayo wacha niende zantel
 
Dah! MAmbo ndo hayo wacha niende zantel
Nakuhakikishia utakuja na mrejesho kuwa siku zote ulikuwa wapi? Zantel ni sawa na kumpata demu bikra miongoni mwa ma Slayqueen πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Kuhusu vocha we jitumie salio kwenye ezy pesa (hii ni kama Mpesa ya Zantel) kisha unajiunga vifurushi juu kwa juu.
 
Hivi kuna watu bado mnakomaa na voda mimi kitambo natumia huu mtandao kupokea tu bando nanunua kupitia halopesa
 
Sasa kwa dar sisi wa ubungo mbez kimara tutapata wapi line za zantel?
 
Halafu data za vodacom zinaisha haraka balaa.
Jana nimeunga kifurushi cha gb 7 lengo kinivushe wiki cha ajabu baada ya masaa kama 6 nacheck salio zimebak 3.2gb, wakati tigo 7 gb natumia kwa wik 2
Inategemea speed ya intaneti. Tigo na Airtel lazima upige revolutions za kutosha kabla ya kupakua ama kufungua media yako. Sasa hasara iko wapi???
 
Inategemea speed ya intaneti. Tigo na Airtel lazima upige revolutions za kutosha kabla ya kupakua ama kufungua media yako. Sasa hasara iko wapi???
Hapana kwa hili nakataa mkuu spid haitofautian sana ukizingatia tigo nina tumia 4G na voda natumia lain ya 3G. Ila cha kushangaza 7gb za tigo nimetumia kwa siku 14 ila hiz za voda ndani ya masaa takriban 6 tu nimetumia Gb 3.9 na wakati matumiz yalikuwa ya kawaida kama siku zote.
 
Basi jaribu kufanya research ya kutosha isiwe to insidenti ya siku moja ukaleta hitismisho. Unaweza kuwa ulichofanyia data za Tigo na Vodacom ni tofauti, kuna pia background applications, updates huwa zinakula Mbs balaa. Nachojua Tigo & Airtel ni VERY SLOW. Vodacom ndo Sisiemu aiseee. Sijajaribu Halotel na Zantel labda nitashawishika kwa maelezo kidogo ya Extrovert
 
Vodacom ni "AZAM TV" wa kwenye Simu,
Sijui hata wanaowasimamia hawa wanafanya kazi gani,
Watu wanajipangia tu bei hakuna wa kuwafanya chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…