VODACOM boresheni huduma siyo matangazo!

VODACOM boresheni huduma siyo matangazo!

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Kampuni ya simu ya Vodacom imekuwa na makeke ya kutangaza biashara yao mpaka imekuwa kero. Mara bajaji, baiskeli, jahazi, kubadili rangi - kazi ni kwako...! Binafsi nilitegemea kwamba hata huduma kwa wateja wake zingeboreshwa ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya simu. Lakini mambo ni yaleyale, hivyo kunifanya niamini kwamba hiyo ni janja ya kuwaibia watanzania kwa kuwadanganya kwa wingi na uzuri wa matangazo yasiyo na tija.
 
ungekuwaq karibu ningekupa tano!!

ila kwakuwa uko mbali ona ninayokugongea (like)
 
Kampuni ya simu ya Vodacom imekuwa na makeke ya kutangaza biashara yao mpaka imekuwa kero. Mara bajaji, baiskeli, jahazi, kubadili rangi - kazi ni kwako...! Binafsi nilitegemea kwamba hata huduma kwa wateja wake zingeboreshwa ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya simu. Lakini mambo ni yaleyale, hivyo kunifanya niamini kwamba hiyo ni janja ya kuwaibia watanzania kwa kuwadanganya kwa wingi na uzuri wa matangazo yasiyo na tija.

Kweli mkuu. Halafu migharama yote hiyo inaelekezwa kwa wateja. Pamoja na kuwepo taasisi ya fair competition mambo yapo gizani sana hasa kwa upande wa mlaji/mteja
 
Hawa jamaa ni kati ya mafisadi gharama kubwa hazilingani na huduma wanazotoa simu hazisikiki mikwaruzo kibao,labda wameshindwa na kuamua kuuza kwa waingereza VODAFONE
 
Hiyo ni kweli kabisa wakuu hawa VODACOM hawana urafiki hata kidogo na wateja wake, unapiga simu unaangalia salio mpaka unatetemeka hayo sio maisha, na ukijichanganya kwenye internet bundles zao ndio utapata presha.
 
walijivua gamba la njano sasa hili jekundu ni balaa tupu
 
Kula tano mtoa mada !! Naichukia vodacom basi tu sina jinsi
 
kwani maana ya kazi ni kwako ni nn wadau maan kila ninaposikia tangazo la vodacom huwa nashindwa kuelewa kabisa
 
Kula tano kiongozi! Simu yangu ina neno "Kazi ni Kwako" ambalo halitoki. Je, kwa mtindo huu naweza kuwashitaki hawa jamaa wa Voda kwa kuniwekea tangazo ambalo silihitaji?
 
Kula kumi kiongozi! Simu yangu ina neno "Kazi ni Kwako" ambalo halitoki. Je, kwa mtindo huu naweza kuwashitaki hawa jamaa wa Voda kwa kuniwekea tangazo ambalo silihitaji?
 
  • Thanks
Reactions: Aza
nami natoa tano kwa mtoa mada, vodacom gharama ni kubwa mno compared to tigo....naipenda tigo...
 
na zile meseji zao,mbona wanatukera?
kwanini kututumia mimeseji ya "charlie chaplin"sijui upupu gani tena usiku
ivi aya mabahati nasibu yao wanafikiri kila mtu anacheza?
watoe matangazo yao ktk simu zetu
 
Back
Top Bottom