tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,133
- 280
Kampuni ya simu ya Vodacom imekuwa na makeke ya kutangaza biashara yao mpaka imekuwa kero. Mara bajaji, baiskeli, jahazi, kubadili rangi - kazi ni kwako...! Binafsi nilitegemea kwamba hata huduma kwa wateja wake zingeboreshwa ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya simu. Lakini mambo ni yaleyale, hivyo kunifanya niamini kwamba hiyo ni janja ya kuwaibia watanzania kwa kuwadanganya kwa wingi na uzuri wa matangazo yasiyo na tija.