Vodacom kuanza kuuza hisa Machi 9

Tena ukisoma vizuri hio tofaut ya faida ilisababishwa na hasara kwenye kampuni yake ya minara Helios Towers ambayo wameamua kuuza hisa zao na kuachana nayo,vinginevyo ni uwekezaji mzuri sana,tukizubaa tutakuja sikia baadae akina Manji ndio wana hisa za kutosha huko na kama kawaida yetu tutalalamika kana kwamba tulikatazwa kuwekeza wakati fursa tulipewa tukaipuuzia.
 
makampuni na taasis za serekali kama NSSF, PSPF Na mabenki ndio hununua hisa nyingi watanzania wa kawaida ni wachache
 
i think hujaelewa kuhusu matket share ilivyotumika. Hapa walimaanisha ile mobile subscribers wa vodacom katika watz wote ni 31% put of 100 then the 8 companies get their shares from the remaining 69%.
so inamaana watje wengi ni wa vodacom.
 
ila mimi bado nahsi ni ghali kidogo na sijui zinaeza kwenda mpaka wapi kwasasa
 
Hallo vipi hawa voda wezi sana unajua ? Msidanganyike bora ununue kwa njia ya bank kuliko mtandao waooo mnaibiwa wakuuu nimepigwa buku tano ya fasta kujisajiri tu ...
Pole sana mkuu!
 
Vodacom hawajawahi kufikisha market share 50%
 
Napendekeza wenye ufaham zaidi na waliochambua prospectus has financial statements watuelimishe zaidi kidogo.
 
Mkuu si ghali kama unavyofikiri. Swissport alianza kuuza kwa Tshs. 225 kwa hisa mwaka 2003 leo anauza kwa Tshs. 5,400.
Hivi unaruhusiwa kununua kwa installments?Mfano ununue kadhaa wiki hìi halafu ununue tena nyingine wiki ijayo?
 
Ukiangalia kesi nyingi Vodacom,TRA na wengineo kama wafanyakazi kama wakishindwa ni zaidi ya billion 100. Faida ya 124bn 2014 na kushuka mpaka 32bn mwaka 2015 hapa na mashaka kidogo kama ni hiyo minara peke yake.
 
Hivi unaruhusiwa kununua kwa installments?Mfano ununue kadhaa wiki hìi halafu ununue tena nyingine wiki ijayo?
Yah inaruhusiwa kaka. Kiwango cha chini ni hisa 100 so unaweza kununua kidogo kidogo mpaka soko litakapofungwa tarehe 19 april.
 
Ukiangalia kesi nyingi Vodacom,TRA na wengineo kama wafanyakazi kama wakishindwa ni zaidi ya billion 100. Faida ya 124bn 2014 na kushuka mpaka 32bn mwaka 2015 hapa na mashaka kidogo kama ni hiyo minara peke yake.

Mhh...hilo nalo neno!@ Babu wa Loliondo na NIMITZ naomba mtufafanulie huku kushuka kwa faida sharp kiasi hiki.
 
Naombeni kufaham kwa hiyo ukiwa n hisa 100 ambayo ni kiwango cha cchini gawio huja kiasi gani?na je huwa hakhna magawio kwa kila mwezi?
 
Naombeni kufaham kwa hiyo ukiwa n hisa 100 ambayo ni kiwango cha cchini gawio huja kiasi gani?na je huwa hakhna magawio kwa kila mwezi?
Gawio sio kama mshahara utaupata kila mwezi,bali gawio hulipwa mwisho wa mwaka baada ya kampuni kujua faida kias gani imepatikana baada ya kulipa kodi,na kiwango chake hutegemea na ukubwa wa faida kwa huo mwaka husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…