Vodacom Kulikoni? TCRA hebu tuokoeni na hizi gharama za Data

Vodacom Kulikoni? TCRA hebu tuokoeni na hizi gharama za Data

Granite

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
268
Reaction score
624
Nilizoea kujiunga Vifurushi vya aina mbili vya wiki 2Gb kwa Tsh.3,000/= au 4Gb kwa Tsh.5,000/= Leo nimekutana na hali tofauti, 1Gb kwa 3,000/= na 2GB kwa 5,000/= kwa kweli nimechanganyikiwa kidogo hasa ukiangalia hali tunayoipitia mtaani.

Mbona hii mitandao imekuwa na upandishaji wa gharama kiholela tu? Huku tunakokwenda sio kuzuri jamani.

Hebu TCRA ingilieni kati na Mamlaka za kulinda haki za wateja.
 
Halotel ni the best kwenye bando na hua haliwai kukata sasa wewe fikilia sms 5000 kwa mwezi tsh 1000 hawa hewateli 1000 sms 1000 kwa mwezi Voda sasa ndo usipime 2000 sms kwa mwezi tigo 1500 sms kwa mwezi.Halotel waki improve kasi yao ya internet vijijn kama voda itakua raha sana.
 
Airtel zile MB 500 zinakata fasta unaweza hisi simu ina tobo mpaka kuna muda najisachi mfukoni kuangalia huenda zilidondokea mfukoni.

Bora 1GB na kuendelea zinavumilia.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
haloteli ni the best kwenye bando na hua haliwai kukata sasa wewe fikilia sms 5000 kwa mwezi tsh 1000 hawa hewateli 1000 sms 1000 kwa mwezi Voda sasa ndo usipime 2000 sms kwa mwezi tigo 1500 sms kwa mwezi.Halotel waki improve kasi yao ya internet vijijn kama voda itakua raha sana.
Utamu wa halotel ni kuwa, muda wa bando ukiisha bando linaonekana limeisha, ila ukinunua lingine lile bando lililobaki(mf MB) zinajumlishwa na hizi ulizonunua upya.

Hapa nilipo nina SMS 58,875 ambazo muda wake unaisha kesho(huwa nanunua kwa wiki kwa 475/= kupitia Halopesa, kwa salio la kawaida ni 500/= unapata sms 3,000).

Kesho sms zikiisha halafu nikinunua zingine zitajumlishwa na hizi 58k ambazo bado zipo(lakini sitaweza kuzitumia endapo muda wake ukiisha).
 
Nilizoea kujiunga Vifurushi vya aina mbili vya wiki 2Gb kwa Tsh.3,000/= au 4Gb kwa Tsh.5,000/= Leo nimekutana na hali tofauti, 1Gb kwa 3,000/= na 2GB kwa 5,000/= kwa kweli nimechanganyikiwa kidogo hasa ukiangalia hali tunayoipitia mtaani.

Mbona hii mitandao imekuwa na upandishaji wa gharama kiholela tu? Huku tunakokwenda sio kuzuri jamani.

Hebu TCRA ingilieni kati na Mamlaka za kulinda haki za wateja.
Wamepewa maelekezo na serikali ya wanyonge watunyonge mpaka tujute kuzaliwa.
 
Back
Top Bottom