vodacom na afande kova

vodacom na afande kova

Mjasiria Akili

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
823
Reaction score
372
hivi ni sahihi afande kova kutumia cheo chake kufanya tangazo la mpesa linaroruka radioni?
 
Yuko sahihi, anawashauri wafanyibiashara waache kutembea na mabulungutu na Vodacom wana hiyo facility. Ulitaka aseme tigo wakati hawana!
 
Ametumia cheo vibaya kujinufaisha ama kwa fedha ua kimaarufu.
 
Alichofanya Kova ni kuweka wazi ukweli kwamba viongozi na watendaji wengi Tanzania wanatumwa na wanalipwa na watu na makampuni binafsi na wamefika mahali hawana hata aibu kujitangaza. Pinda naye huwa anavaa T-Shirt za hawa Vodacom katika shughuli zake. Viongozi na watendaji wetu wana bei-wananunulika na wanatumika, tunasubiri siku PV ya posho aliyoewa Kova iwekwe hapa. Katika mazingira haya maslahi ya wananchi au umma kwa ujumla siyo ya msingi.
 
Hv tunashindwa kuelewa kuwa hata Kova naye ni binadamu kama wewe na mimi!
 
Kwani kuna ubaya wowote?

Seconded - Je kuna ubaya wowote? Vodacom na washindani wake ni Vyama vya Siasa? Airtel, Tigo, Zantel, etc. waliwahi kumfuata akakataa?

Vipi kuhusu lile Tangazo linalotoka mara kwa mara "la kuhamasisha Amani Tanzania" linalotolewa "kwa Hisani ya Radio One Stereo" kupitia Radio One Stereo likihusisha kila mmoja kivyake akina Afande Mwamunyange, Sheikh (sorry simkumbuki jina), Kardinali Pengo, Mhindi fulani, n.k. Mbona hakuna aliyewahi kuhoji kuhusu ushiriki hasa wa Mwamunyange kwenye Tangazo hilo?

Double Standards, Wakuu?
 
hivi ni sahihi afande kova kutumia cheo chake kufanya tangazo la mpesa linaroruka radioni?

Kova kasema kwa Niaba ya jeshi la polisi so ni sahihi kabisa

ni sawa sawa
kova huyu huyu akwambie kuweka pesa majumbani si salama weka benki

so ni sahihi kabisa

ila kuna watu wanamawazo ya kipinzani pinzani ndio wanataka kuleta shida otherwise hakuna shida yeyote
 
watanzania tunachosha mbaya mazee coz kilakitu tunalala mika tu sasa mnataka hilo tangazo ange pewa babako aliadivatise au ndo hivi viumbea umbea vya ukubwani fata mambo yako raster
 
Hv tunashindwa kuelewa kuwa hata Kova naye ni binadamu kama wewe na mimi!

...Naam, Mkuu! Ni binadamu kama wewe na Mimi lakini tofauti na mimi na wewe yeye tumemkabidhi Ofisi ya Umma kwa kusimamia na kulinda Masilahi ya Umma!

Kama alikuwa na Nia ya kweli ya kutaka Watzanzia wasiibiwe Fedha zao basi alipaswa kuyataja makampuni yote yenye Huduma hiyo kama vile TigoPesa, AirtelMoney na ile ya Zantel.

Kutaja Kampuni moja tu ni wazi kuwa Mheshimiwa sana Kova ametanguliza Maslahi binafsi Mbele kwa kutumia Ofisi ya Umma.

Kwa maneno mengine ni kuwa Itakapofika mahali TigoPesa, Airtel Money na Mpesa watakapohitaji huduma ya aina moja na wakati mmoja kutoka kwa Mheshimiwa Kova, huhitaji kuumiza akili kujua kampuni ipi itapata Upendeleo wa Huduma za Mheshimiwa Kova kwa kutumia Ofisi ya Umma.
Kuna wakati fulani Viongozi wa Umma wanatakiwa kuwa above siasa za ushindani za makampuni yanayotoa huduma kwa Watanzania.
Katika hili Mafisadi utawajua tu.

:suspicious:
 
Kova kasema kwa Niaba ya jeshi la polisi so ni sahihi kabisa

ni sawa sawa
kova huyu huyu akwambie kuweka pesa majumbani si salama weka benki

so ni sahihi kabisa

ila kuna watu wanamawazo ya kipinzani pinzani ndio wanataka kuleta shida otherwise hakuna shida yeyote

...Mkuu, Kwa maana hiyo Jeshi la Polisi linaitambua Mpesa tu kwamba ndio Kampuni Pekee inayotoa Huduma ya kutuma na kupokea fedha?
Kwa nini kama Jeshi la Polisi lina Nia Njema lisitaje Makampuni yote Manne ya Simu yenye huduma ya kutuma na Kupokea fedha?
Huoni kwamba kwa kuitaja Mpesa tu Afande Kova/Jeshi la Polisi linakuwa limetumika kutoa advantage kwa kampuni moja dhidi ya nyinginekatika nyakati hiz ngumu za Ushindani wa Kibiashara?
Mbona hili lilihitaji Utashi wa Kawaida tu kwa Mheshimiwa Kova kujiepusha kuonekana kuipigia debe kampuni moja dhidi ya nyingine??
Kwa nini Viongozi wetu wajirahisisha hivi??????

Seconded - Je kuna ubaya wowote? Vodacom na washindani wake ni Vyama vya Siasa? Airtel, Tigo, Zantel, etc. waliwahi kumfuata akakataa?

Vipi kuhusu lile Tangazo linalotoka mara kwa mara "la kuhamasisha Amani Tanzania" linalotolewa "kwa Hisani ya Radio One Stereo" kupitia Radio One Stereo likihusisha kila mmoja kivyake akina Afande Mwamunyange, Sheikh (sorry simkumbuki jina), Kardinali Pengo, Mhindi fulani, n.k. Mbona hakuna aliyewahi kuhoji kuhusu ushiriki hasa wa Mwamunyange kwenye Tangazo hilo?

Double Standards, Wakuu?

..kama huoni tofauti kati ya tangazo la Amani Tanzania na hilo la Voda basi fanya kitu kimoja .... AMKA!
 
...Mkuu, Kwa maana hiyo Jeshi la Polisi linaitambua Mpesa tu kwamba ndio Kampuni Pekee inayotoa Huduma ya kutuma na kupokea fedha?
Kwa nini kama Jeshi la Polisi lina Nia Njema lisitaje Makampuni yote Manne ya Simu yenye huduma ya kutuma na Kupokea fedha?
Huoni kwamba kwa kuitaja Mpesa tu Afande Kova/Jeshi la Polisi linakuwa limetumika kutoa advantage kwa kampuni moja dhidi ya nyinginekatika nyakati hiz ngumu za Ushindani wa Kibiashara?
Mbona hili lilihitaji Utashi wa Kawaida tu kwa Mheshimiwa Kova kujiepusha kuonekana kuipigia debe kampuni moja dhidi ya nyingine??
Kwa nini Viongozi wetu wajirahisisha hivi??????

Nilijua tu kuna mtu ataniuliza swali hili
anyway
Mbona simple tu vodacom ndio wamemfuata kumuomba ayaseme kama haya aliyoyasema makampuni mengine yamelala usingizi sasatel ndio kafa kabisa vodacom wanajua wanachokifanya wameifuata polisi polisi wakakubali kwani hawajavunja sheria yeyote
wanatangaza best way ambayo ni safe ya kukaa na pesa
laiti kama kova angesema kuwa tutumie mtandao wa vodacom kuwasiliana hapo ingeleta shida

makampuni mengine nayo hayakatazwi kufanya kile ambacho kile vodacom wamefanya
 
1. Tatizo ni Hilo la Kuchukulia Kila Kitu Simple. Inapokuwa hata Viongozi wetu ni Hivyo, Ndio Majanga yenyewe hayo.

2. Kwa hiyo kwako Mkuu CTU Kova kusema 'Tutumie Mpesa kutuma na kupokea fedha' Sio Tatizo ila akisema 'Tutumie Mtandao wa Vodacom Kuwasiliana' ndio Tatizo tu ???

yeye kaongea kwa ajili ya kiusalama hii point ielewe mkuu
ni sawa sawa aseme tumieni bank fulani kuweka pesa na sio majumbani kwenye godoro
 
Seconded - Je kuna ubaya wowote? Vodacom na washindani wake ni Vyama vya Siasa? Airtel, Tigo, Zantel, etc. waliwahi kumfuata akakataa?

Vipi kuhusu lile Tangazo linalotoka mara kwa mara "la kuhamasisha Amani Tanzania" linalotolewa "kwa Hisani ya Radio One Stereo" kupitia Radio One Stereo likihusisha kila mmoja kivyake akina Afande Mwamunyange, Sheikh (sorry simkumbuki jina), Kardinali Pengo, Mhindi fulani, n.k. Mbona hakuna aliyewahi kuhoji kuhusu ushiriki hasa wa Mwamunyange kwenye Tangazo hilo?

Double Standards, Wakuu?

Mkuu unafananisha vitu viwili tofauti. Do you know the difference between Advertising and Public Service Announcement (PSA).

Radio One's Amani campaign ni PSA lengo lake sio kutangaza bidhaa au huduma kwa wateja bali kuelimisha umma juu ya masuala ya amani.

On the other hand Vodacom is advertising its M-PESA service. This is business, the aim is profit. By virtue of his office and public image Kova's endorsment of M-PESA is unethical advertising and favors Vodacom over its competitors.

Hakuna double standards hapo!
 
1. Tatizo ni Hilo la Kuchukulia Kila Kitu Simple. Inapokuwa hata Viongozi wetu ni Hivyo, Ndio Majanga yenyewe hayo.

2. Kwa hiyo kwako Mkuu CTU Kova kusema 'Tutumie Mpesa kutuma na kupokea fedha' Sio Tatizo ila akisema 'Tutumie Mtandao wa Vodacom Kuwasiliana' ndio Tatizo tu ???

Jamaa anamiss point. Inawezekana ni tatizo la elimu ya uraia. Mkuu CTU, Hata kama Kova alifuatwa na Vodacom hakupaswa kukubali kwa sababu ya nafasi aliyonayo katika jamii.

Angekuwa mbele huko kampuni nyingine zingeshamshtaki. Ni uzembe ambao umezoeleka na sasa unaonekana ni kitu cha kawaida.
 
Back
Top Bottom