Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mimi ni mtumiaji na mteja wa miaka mingi wa mtandao wa voda ,lakini Haijawahi kutokea na sijawahi kushuhudia hali hii katika simu yangu ya ulaji wa mb utafikiri kuna jini limepiga kambi kula mb zangu. Hali hii imejitokeza tangia jana jioni ambapo nilikuwa na mb mia mbili na 34 lakini ghafla nikashangaa naletewa sms kuwa zimekwisha.
Nilipigwa na mshangao mkubwa sana.baadaye nikasema ngoja nijaribu niweke mb za mia tano.nikaweka nikapewa mb 246 cha kushangaza nikaingia jamii forum na kukaa kama dakika tatu au nne hivi bila kufungua video ya aina yoyote ile.lakini nikaletewa sms kuwa zimebaki mb 61.
Lakini cha kushangaza baada kama tena ya dakika 2 hivi nikaletewa sms kuwa kifurushi chako cha JKU kimekwisha.Nilishangaa sana na kusikitika sana hali hiyo.
Nimepiga sana huduma kwa wateja bila kupata msaada wa aina yoyote ile,kwa kuwa sikupata nafasi ya kuongea na wahudumu wa voda zaidi ya kupewa maelekezo ya kujihudumia mwenyewe.
Sasa muda huu tena nimejiunga bando la mia tano na kupewa mb 246 hivi lakini cha kushangaza nimeingia tu JF na kukaa kama dakika mbili bila kufungua video au kuandika chochote wala kusoma habari hata moja zaidi ya kuangalia nyuzi tu.nikasema ngoja nikaangalie salio,nikakuta tena salio eti ni mb 110 .
Wakati hali hiyo haijawahi kutokea. Sasa najuwa humu jukwaani wapo voda nataka kujuwa shida ni nini?