Vodacom Premier League 'VPL' Alliance FC Vs Simba SC, Furaha Kwa Wanasimba Uwanja wa Kirumba

Vodacom Premier League 'VPL' Alliance FC Vs Simba SC, Furaha Kwa Wanasimba Uwanja wa Kirumba

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, Kuendelea kupigwa tena leo January 19, 2020 ambapo Alliance FC, wakiwa nyumbani wanawakabili Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezo wa leo huenda ukawa ni mgumu kwavile kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiimarisha kwenye msimamo wa VPL, huku wenyeji Alliance FC wakiingia na kumbukumbu ya kutopata matokeo mazuri kwa Simba SC, ambapo katika mechi mbili walizokutana Alliance FC waliambulia kichapo cha mabao 5-1 kwenye dimba la Taifa kabla ya kuchapwa tena 2-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Je Alliance FC atafuta unyonge kwa Simba? Au Simba SC ataendeleza ubabe wake? Muda utaongea usikae mbali Ukakosa Ukaambiwa kuanzia saa 10:00 alasiri.

===========••••============

Simba SC ikicheza kandanda safi imeibuka na ushindi mnono wa mbao manne kwa moja dhidi ya Alliance FC ikiwa ni mfululizo wa VPL, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Alliance FC walikuwa wakwanza kuandika bao katika dakika ya 27' likifungwa na Israel Patrick

Simba walisawazisha kabla ya mapumziko likifungwa na Jonas Mkude 45+3' kipindi cha pili kilianza kwa kushuhudia mabao ya Kagere 58' Chama 64' Dilunga 73' akihitimisha hiyo kalamu ya mabao.

Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kujikita kileleni kwa kukusanya alama 41 ikicheza michezo 16 kwenye msimamo wa VPL.

FT: Alliance FC 1-4 Simba SC

tapatalk_1579434457679.jpeg
IMG_20200119_144449_343.jpeg
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, Kuendelea kupigwa tena leo January 19, 2020 ambapo Alliance FC wakiwa nyumbani wanawakabili Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.View attachment 1327514View attachment 1327515
Manara anawadanganya sana..Mkia sio bingwa ni bingwa mtetezi (defending champion)
 
Mnyama nguvu Moya.
Afwazali Manula na Mzamiru tumewapiga likizo ya lazima katika kikosi cha kwanza maaana siyo kwa kutukosea heshima kiasi kile tarehe 4
 
00' Timu zote zipo uwanjani wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Kirumba


Naaaaaaam mpira umeanza ligi kuu ya Vodacom Premier League

Alliance FC 0-0 Simba SC
 
05' Timu zimeanza kwa mashambulizi makali huku Simba wakilifikia lango la Alliance FC mara tatu dhidi ya mara moja na Simba wakipata kona ambayo haikuzaa bao

Alliance FC 0-0 Simba SC
 
Back
Top Bottom