Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, Kuendelea kupigwa tena leo January 19, 2020 ambapo Alliance FC, wakiwa nyumbani wanawakabili Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mchezo wa leo huenda ukawa ni mgumu kwavile kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiimarisha kwenye msimamo wa VPL, huku wenyeji Alliance FC wakiingia na kumbukumbu ya kutopata matokeo mazuri kwa Simba SC, ambapo katika mechi mbili walizokutana Alliance FC waliambulia kichapo cha mabao 5-1 kwenye dimba la Taifa kabla ya kuchapwa tena 2-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Je Alliance FC atafuta unyonge kwa Simba? Au Simba SC ataendeleza ubabe wake? Muda utaongea usikae mbali Ukakosa Ukaambiwa kuanzia saa 10:00 alasiri.
===========••••============
Simba SC ikicheza kandanda safi imeibuka na ushindi mnono wa mbao manne kwa moja dhidi ya Alliance FC ikiwa ni mfululizo wa VPL, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Alliance FC walikuwa wakwanza kuandika bao katika dakika ya 27' likifungwa na Israel Patrick
Simba walisawazisha kabla ya mapumziko likifungwa na Jonas Mkude 45+3' kipindi cha pili kilianza kwa kushuhudia mabao ya Kagere 58' Chama 64' Dilunga 73' akihitimisha hiyo kalamu ya mabao.
Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kujikita kileleni kwa kukusanya alama 41 ikicheza michezo 16 kwenye msimamo wa VPL.
FT: Alliance FC 1-4 Simba SC