Hakuna timu isiyofungwa duniani. Tena mara nyingi timu kubwa hufungwa na timu vibonde. Kwa Simba hii ni "wake up call" kuwa ligi ya mwaka huu sio nyepesi. Kama wanataka ubingwa wajipange hasa.
Lakini goli la jana la Mwadui halinishangazi sana kwani ni aina ya magoli anayofungwa Manula kila mara. Mara nyingi anakuwa na kiherehere cha kusogea hatua kadhaa mbele ya goli pasipo sababu ya msingi. Ndio maana Kaseja atamburuza sana kwenye timu ya taifa mpake aote mvi ndio Manula atakuja kupata nafasi tena ya kucheza timu ya taifa. Huwa najiuliza kocha wa makipa pale Simba bwana Muharami ameshindwa kabisa kumrekebisha Manula kwenye haya mapungufu ya kusogea hatua kadhaa mbele ya goli bila sababbu za msingi? Halafu Ndairagije akimwacha kwenye timu ya taifa mashabiki wanapiga kelele bila kujua mapungufu ya Manula ni nini ukimlinganisha na Kaseja.
Jambo la pili ni timu nzima ya Simba iache kudharau baadhi ya timu. Najaribu kuangalia jinsi Simba ilivyocheza mechi mbili na Azam (ligi na ngao ya jamii) na jinsi ilivyocheza na Kagera Sugar mwanzoni mwa ligi hapo Simba walikuwa bora sana. Halafu naiangalia Simba iliyocheza na Singida United pale Arusha pamoja hii ilivyocheza na Mwadui. Utaona kabisa baada ya Simba kushinda mechi za mwanzo basi wakaridhika. Kuanzia mchezo na Singida na huu wa Mwadui Simba walikuwa wanacheza tayari na matokeo mkononi' Hata Singida wangetulia wangeweza kushinda ile mechi ya Arusha kama walivyofanya wenzao Mwadui jana.
Ni wakati sasa Ausems na benchi zima la ufundi la Simba kufanya "rotation" kwa golikipa kama wanavyofanya kwenye nafasi nyingine ndani ya uwanja ili kuleta ushindani na kuondoa dhana ya mtu kumiliki namba.