Vodacom Premier League ' VPL' Simba SC dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Kulitaka Mwana!

Vodacom Premier League ' VPL' Simba SC dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Kulitaka Mwana!

64' Ametoka Jonas Mkude na ameingia Mzamir Yassin, upande wa Simba SC
 
Anapiga shuti Michael Gadiel go laa..Golikipa anadaka bila wasiwasi

Ametoka Omari na ameingia Nassoro upande wa Ndanda FC
 
77' Ametoka Ibrahim Ajibu na nafasi yake amechukua Clatuos Chama, upande wa Simba SC

Bado mpira unachezwa sana eneo la kati huku Simba wakijaribu kuzidisha mashambulizi na Ndanda wakijibu

Simba SC 1- 0 Ndanda FC
 
Makasi anapiga free kick, lakini Aishi Manula anadaka, ilikuwa nafasi ya kusawazisha kwa Ndanda
 
Goooooooooooooooooooaaal Goooal

Deo Kanda anaipatia Simba SC bao la pili baada kuugusa mpira na kujaa wavuni ambao uliopigwa na Gadiel Michael

Simba SC 2-0 Ndanda FC
 
90+2' kuelekea kumalizika kwa mchezo, ambapo Simba wanaongoza kwa bao mbili

Dakika chache wachezaji wa Simba wakigonga pasi za hapa na pale huku Gadiel na Ndemla wakikosa nafasi ya kuipatia Simba bao la 3.

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umekwisha ambapo Simba wametoka kifua mbele kwa mabao mawili bila majibu yakiwekwa kimiani na Kahata dakika ya 13, na Deo dakika ya 85.

FT: Simba SC 2- 0 Ndanda FC

•••••Ghazwat......
 
Simba wameniangusha goli moja tu nilikuwa nalihitaji waongeze.
BTW Viva Msimbazi
 
90+2' kuelekea kumalizika kwa mchezo, ambapo Simba wanaongoza kwa bao mbili

Dakika chache wachezaji wa Simba wakigonga pasi za hapa na pale huku Gadiel na Ndemla wakikosa nafasi ya kuipatia Simba bao la 3.

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umekwisha ambapo Simba wametoka kifua mbele kwa mabao mawili bila majibu yakiwekwa kimiani na Kahata dakika ya 13, na Deo dakika ya 85.

FT: Simba SC 2- 0 Ndanda FC

•••••Ghazwat......
Nimepitwa aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, unaanza kuipangia Simba wanaotakiwa kucheza? Hapo kocha alifumba macho tu akaokota vikaratasi vyenye majina, yaliyookotwa ndio hao unaowaona wamepangwa
Ila Leo wamecheza mpira mbovu mno sio Simba ninaowajua.
 
Ina maana wakuu Laki Si Pesa, Shadeeya nk nk hawana hela ya kununua mb au hawaiamini timu yao?
Tatizo muda Mkuu. Sababu mipira mingi huwa inaanza ile mida ambayo nakuwa busy na mambo mengine nje ya Jf.

Pia kama muda ninao naleta updates kwenye uzi wa Timu ya Wananchi.
 
Tatizo muda Mkuu. Sababu mipira mingi huwa inaanza ile mida ambayo nakuwa busy na mambo mengine nje ya Jf.

Pia kama muda ninao naleta updates kwenye uzi wa Timu ya Wananchi.
Sawa mkuu, majukumu yetu ya kimaisha ni kwanza ila mbona sio wote? Ukweli ni kuwa hamuiamini kabisa timu yenu ndio maana mara zote mnajitokeza kwa kasi baada ya mpira kuisha kuwasaidia mnakuwa na matokeo tayari.
 
Oooh. Kwa kuwa umeshajiaminisha hivyo mimi ni nani mpaka nikubishie Mkuu.

Nikukumbushe leo ni Januari 02 2020
 
Oooh. Kwa kuwa umeshajiaminisha hivyo mimi ni nani mpaka nikubishie Mkuu.

Nikukumbushe leo ni Januari 02 2020
Sawa mkuu, imebaki kesho tu, Jumamosi tunawashikisha adabu.
 
Back
Top Bottom