Nimewasikia wachambuzi wa Azam Sport wamesema yafuatayo;
a) kocha wa Simba huwa hafanyi research kuhusu timu anayocheza nayo ubora wao ni upi na yeye achezeje, yeye anafanya rotation zake tu bila kujua hii ni mechi gani. Na hii inathibitishwa na kauli yake baada ya mchezo kuwa Prison walidefend na kufanya counter hivyo ikawa vigumu kwa Simba kucheza.
b) Kocha wa Prison alijua Simba wanachezaje na yeye acheze vipi
c) Mchezaji kama Miraji Athumani anafanya vizuri sana anapoingia kucheza kuliko wachezaji wengi ambao kocha amewafanya ni regular players, na hivyo inamchanganya anapokuwa anamiweka benchi au kumuweka kwa kipindi kifupi.
d) Upangaji wake wa timu na subs ni mgogoro, leo kamtoa Ajib ambae ni striker aliyekuwa anatakiwa kusaidiana na Kagere, amemuacha Mzamiru na Fragha kwenye game tough.
Kiukweli hata mimi simuelewi huyu kocha wetu, ni wa mpira au tuliingia chaka.