Nimeona watu wengi wanalalamika sana kuhusu aina ya mpira ambao Simba inacheza kwa kipindi hiki. Ni kweli hata mimi siridhishwi na aina ya uchezaji huu hasa kipindi cha kwanza. Angalau kidogo kipindi cha pili timu inacheza na kushambulia...
Hii yote inasababishwa na aina ya kikosi ambacho huwa kinaanza kwenye mechi husika. Simba katika mechi za hivi karibuni kila mechi kikosi kinakuwa na wachezaje tofauti tofauti, leo kaanza huyu kesho yule kesho kutwa yule kule, kwa sababu hii maelewano au chemistry kwenye timu inakosekana, na ndio maana kadri siku zinavyozidi kwenda timu kupata matokeo inatumia nguvu nyingi sana... tatizo ni chemistry kwenye timu, hili ndio tatizo.