Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Tunapiga masaa mia tanotumesubr ttkuwa tunatenga ck kwaajir yakuongea na nyny?
Pole snaa Thino, ni kwamba wakati unapiga kunakuwa na wateja wengi wanaohudumiwa hivyo tunaomba uvumilivu wako, unaweza pia kupiga namba 15366 ambayo ni ya haraka zaidi.
 
Voda achen ujinga nimenunua dk 4 mitando yote na nlkua na dk 50 Voda 2 Voda xa iv mnanambia dk zmeisha nahama mtandao ata kama ndo kutuona wajinga cio my no0764463202
Habari KPClassic tafadhali tunaomba namba ya simu kwa msaada zaidi.
 
Naomba maelekezo namna ya kujiunga Na vifurushi vya kimataifa Na kwa mini nikipigiwa SIMU nakatwa salio?
Habari Ziege, bado tunafanyia marekebisho vifurushi hivyo ndugu mteja. Ukipigiwa simu unachajiwa kwasababu unatumia namba yako nchi nyingine ambapo anayekupigia huchajiwa gharama ya kawaida kana kwamba kapiga simu kwa mtu aliyepo nchini na wewe hutozwa gharama za ziada kuunganisha simu hiyo kimataifa. Ahsante
 
Mmenikera sana mnauza voda foni smart 80 alafu mnatuambia unapata 3gb kwa miez 6 alafu mnatoa mb 200: nyie no wezi na nimejuta kupoteza 80 yangu, alafu nashangaa tcra inaacha swala hili, mnatuibia watanzania mchana kweupe, cwapenda na ninawachukia mpaka basis, hata lazima tupige kampeni tuwasuse mmekua wezi sana na sijui kama mnalipa kodi kisawasaw, nyie no janga LA kitaifa.

Habari Mungumaji, kifurushi cha 3GB kinatolewa kwa miezi 6 ambapo kila mwezi mteja anapata 500MB.
 
Bundle ikikaribia kwisha alert yenu inachelewa nakuta nimeliwa salio langu lote kwa muda mfupi sana pia Kuna vocha inagoma ya buku mbili nisaidieni ikubali pm niwape namba
Habari Dizzle, ujumbe wa kumfahamisha mteja kuwa kifurushi kimeisha hutumwa, tunaomba namba ya simu kuangalia suala hili na tutakupatia jibu.
 
Voda ni wehu wanatubadilishia bando yani wanataka kutulazmisha matumiz sio fair ivo kumbukeni voda ndo mtandao uliotapakaa mpk vijijini mnawatesa walalahoi.
Kwel naamini kua vodacom kazi ni kwetu.na tutahamaa

Habari Prudnc, mabadiliko yanapotokea huwa ni katika kuendena na kile ambacho wateja wanahitaji zaidi. Na mara nyingi hufanywa hivi kwa maboresho. Tungependa kufahamu bando ipi unayoizungumzia.
 
0756525889 Kwanini haipati mkopo na M.PAWA hata nikiweka akiba????? USAJILI WOTE NIMEKAMILISHA.
 
Watumiaji wengi wa simu siku hizi tunatumia smartphone jambo ambalo linafanya uhitaji wa data bundle zaidi...nawapa ushauri kama mnaweza fanyeni kutoa mb zaidi ya sms nyingi ambazo hazina maana
 
Duh....customer care shughuli aiseee.......lakini hiki ndio kioo halisi mtaani.....
 
Nime nunuwa umeme kwa njea ya luku kwenye namb 0752589656 saa 7:42 mpaka sahizi ujanipa majibu
 
Habari Dizzle, ujumbe wa kumfahamisha mteja kuwa kifurushi kimeisha hutumwa, tunaomba namba ya simu kuangalia suala hili na tutakupatia jibu.


Voda acheni uongo yani mnatuma sms bado limeishaisha hadi salio mmeshakata nyie mnaudhi sana
 
Habari Prudnc, mabadiliko yanapotokea huwa ni katika kuendena na kile ambacho wateja wanahitaji zaidi. Na mara nyingi hufanywa hivi kwa maboresho. Tungependa kufahamu bando ipi unayoizungumzia.


Yani kupunguza mb 100 hadi mb 50 ndiyo mnasema kulingana na wateja acheni huo wizi wa mchana hv hata hamjishitukii hebu chekini AIRTEL na TIGO
 
Hizi kampuni za Akiba Saccos na community loan ni matapeli kwann mmewaruhusu kutumia lines zenu?
 
Back
Top Bottom