Ni muda sasa mtandao au kampuni ya vodacom imekuwa ikilalamikiwa na wateja wake kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo katika kampuni hiyo hasa pale ambapo salio la mtu lilipokuwa likikatwa na unapopiga simu huduma kwa wateja,muhudumu anakwambia kuwa salio lako limetumika kwa kuwa hukuzima data katika simu yako.
Hapo ndipo mwanzo wa wizi na hujuma za vodacom zilipoanza kwani iliwezekanaje simu iwe na kifurushi cha kutosha,MB za kutosha DAKIKA za kutosha na SMS za kutosha halafu mwisho wa siku uambiwe DATA ktk simu yako ndiyo iliyomaliza salio lako ?
Kwani matumizi ya data kuw on na matumizi ya vifurushi vya voda yanatofauti ?
Imefikia hatua sasa vodacom mshakuwa kero tena kubwa tu,unaweza kupiga simu huduma kwa wateja na muhudumu bila aibu anakwambia umpigie baada ya nusu saa au dakika kadhaa,hapo unaweza kujiuliza kuwa hiyo namba 100 ni line ya mtu binafsi au la ?.
Baada ya malalamiko yote hayo,sasa voda wamekuja na mtindo mpya kabisa ambao kibiashara na wizi na hujuma kwa wateja wao.
Nipo wilaya ya Arumeru,kata ya Akeri na tarafa ya Poli hapa mkoani Arusha.,eneo hili ni zaidi ya wiki sasa unapozungumza na mtu kupitia mtandao wa simu unakuwa hamsikilizani kabisa na mara nyingi tatizo hili linakuwa kubwa hasa nyakati za usiku.
Hapo tunajiuliza,tatizo hili hamlitambui na kama hamlitambui ni kwanini na kama mnalitambua ni kwanini hamjalitatua na kama lipo nje ya uwezo wenu ni kwanini mnaendelea kukata salio wakati mnatambua vizuri kuwa hakuna mawasiliano katika mtandao wenu ?
Ningependa kuwauliza vodacom,hivi mnachofanya mnaelewa kuwa ni wizi na hujuma kwa watanzania na muda si mrefu watanzania watawachoka na kuwafurumushia makwenu ?
Yapo makampuni mengi ya simu yanayotaka kuja kuwekeza Tanzania na pia Tanzania kuna makampuni ya kutoa huduma kwa wananchi.
Bado muda mfupi,wateja wenu tutapeleka malalamiko yetu serikalini na hapo ndipo itakapojulikana mbivu na mbichi.
TUMEWACHO.