Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hivi vodacom mkijifunza na kuiga kwa wenzenu wa airtel mtafilisika? Kwa nini msitoe taarifa ya salio la kifurushi kila baada ya kupiga simu? Ninawapenda lakini mnaniboa sana.
 
Asante saana Vodacom kwa Huduma nzuri mnayotoa...ila mm mwezi ulioisha nilienda Ku renew line nikatoa Tsh- 2500 na kuambiwa ntawekewa 2000 kwenye Salio...lakini sasa mpaka Leo hata 10 sijaiona
 
Mbona university promotion mmeweka kiubaguzi wakati Tigo wameweka vyuo vingi? Au mnapenda kuona wanafunzi wote wanahamia tigo? Au mnafikuri 2taendelea kuwa wanafunzi milele? Mkumbuke 2kishahamia mtandao mwingine ndo ha2rudi tena
 
daaaa! voda kiukweli nmewamaind sana coz dzain kama mnabweteka na idad ya watumiaji wa huu mtandao hebu jiongezen km wale wa... halaf ww beeeeeele
 
Mimi binafsi naipenda sana vodacom lakini sasa hv mtandao unakuwa wa wenye nacho kama huna basi utakushinda mmepandisha bei sana huduma zenu kwakweli, rekebisheni kidogo hapo kwenye bando zenu.
 
huu uzi sidhani kama upo kuwasaidia wateja wa Vodacom nadhani dhumuni thabiti ni kujua watumiaj wa Vodacom jamii forum.
 
Kuna ujumbe huu unaosambaa:

Jamani, nawaomba hiyo namba msipokee had sasa imeuwa watu wawili 0766601665 halafu ukiangalia kwenye m pesa jina linakuja MUNGU SHETANI tafadhari nakuomba watumie wote kwenye sim yako okoa roho za watu kikubwa tukazane maomb asante. NIMEITUMA KAMA NILIVYOTUMIWA.

Na mimi nimeiandika kama ilivyo kwenye inbox exactly, tusaidieni hapa jamani, hiki ni nini?
 
Mwenye kujibu alitakiwa awe Vodacom. Ila nijuavyo ili kupata hela ktk kampuni wakasajili laini kwa jina husika kisha wewe huwezi kumjulisha mtu kama huna salio. Lazima utanunua vocha. Tumsifu Yesu Kristu.
 
Jana nimeweka vocha ya mia 5 ili kujiunga na cheka, matokeo yake kila nikijiunga mnasema sina salio la kutosha nikirudi kwenye account yangu mia 5 ipo pale pale matokeo yake baada ya muda ela ikatumika bila kuunga bundle na hili tatizo limekuwa la kujirudia rudia mara kwa mara, hebu jaribuni kuboresha system zenu jamani tupata hasara
 
Vodacom kazi ni kwako
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Nyie ni kero mimeseji mingi ya promosheni isiyo na tija acheni mtu akitaka kitu asome matangazo siyo kutuma msg kwa kila namba wengine ni kero kwetu
 
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Jamani Nyie, mnasema tutume matatizo huku, mbona hamjibu? Mi nimeuliza kuhusu ujumbe unaosambazwa kuwa tusipokee namba fulani kwasababu imeshauwa wawili na ni hatari, mbona hamjanipa ufafanuzi kuhusu hilo?

Nawashauri msome yale yanayopostiwa na mjibu ASAP, sio poa kutuambia tuulize tutasaidiwa kwa urahisi halafu tunakaa saa zaidi ya 32 hakuna mnachojibu, wajibikeni tafadhali, otherwise don't promise what you cant deliver.
 
Voda hua mtandao wao inasumbua sana sana sana sana sana sana sana sana sana sana sana hasa arusha
 
Namshukuru mungu hata kwa hili
 
Attachments

  • 1428617993688.jpg
    1428617993688.jpg
    71.1 KB · Views: 199
Voda mnaboa sana.. Yani unakuta Internet inasumbuua hata siku tatu.. Cha ajabu hata kutuma sms ya kuomba radhi hakuna. Sasa Sisi tutaota kama mkonga umekatika au..!? . Na hata ukirudi hamrudishi bundle kwa usumbuf. Yani kero sana sio Siri. Mnatuboa wateja.. Hasa mimi Yani.. Nlivyokuwa
 
Text zenyewe haziendi. Unatumiwa text leo unaipata kesho! Yaani kiufupi mmezidisha matangazo ambayo hayana uhalisia. Sms zenu zisizo na tija kwetu ndio kibao.
 
Back
Top Bottom