Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom nawachukia toka moyoni huduma zao za hovyo sana siku hizi..4g haifanya kazi kwangu pamoja na kuwa jjn dsm lakn ni hvyo zaid bora hata tigo wanajali kikubwa nimeshahamia ttcl......ndo baba lao 4g ya kasi zaidi...
 
Kuna wizi mpya umezuka mtaani. Wizi huo umeanza kutokea baada ya tangazo la usajiri mpya wa line za simu kwa kutumia alama za vidole.
Wezi wanapita mtaani wakiwa na sare pamoja na vitambulisho wakisema wao ni watoa huduma za kusajiri line kwa alama za vidole.

Wanachokifanya ni kumwambia mpata Huduma kuwa inatakiwa atume Meseji yenye kiambatanisho cha namba za siri za mpesa kwenda 100. Wao wakiwa na uhakika kuwa Meseji haiwezi kwenda Bali itarudi ikiwa na hizo namba za siri. Hapo ndipo wanapopata mwanya wa kuiba.

Sasa nilikua nataka kujua, kutokana na wizi huu mpya, nyie mmejipangaje kuhakikisha mnawasaidia wananchi kwenye kuibiwa kwa aina hii ya wizi? Namaanisha mmeshaanza kutoa elimu kupitia njia ya Meseji ili wakitokea watu wa aina hii washughurikiwe au mnafanyaje?
 
Hivi hii inshu ya Tusua mapene ipoje?mbona siielewi mimi na hakuna hata mshindi aloyetajwa hadharan kama ilivyo kwa wengine mf:biko n.k
 
Ni aibu sana kwa mtandao mkubwa wa mawasiliano kama Vodacom kutusumbua na kutujazia matangazo yenu kwenye inbox text zetu haswa Mimi ni mwasilika wa hizi text toka Vodacom , sijawahigi kujiunga au kuomba kuunganishwa kwa ajili ya kupata infoz updates za huu ujinga mnaonitumia kila lisaa.
Pls stop this shit om.
Sample text za hawa Jamaa wanituamizo ni kama hizi [emoji116]

Vodacom kama ni brand mnayo hamna haja ya kuendelea kunijazia matangazo yenu haya. Hamnilipi kwa chochote hicho kwa ajili ya hiz promo zenu ispokuwa mm ndo nawaweka mjn hapa kwa kununua vocha zenu.
Acheni huu upuuzi.
 
Tunaomba mtuswapie line zetu za zamani za 3G kwenda 4G badala yakuwa na maline malini mawili mawili.
 
Habarini wa kuu.Naomba mnifahimishe jinsi ya kujitoa kwenye huduma ya. "SOKA LETU" ya vodacom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…