Kuna wizi mpya umezuka mtaani. Wizi huo umeanza kutokea baada ya tangazo la usajiri mpya wa line za simu kwa kutumia alama za vidole.
Wezi wanapita mtaani wakiwa na sare pamoja na vitambulisho wakisema wao ni watoa huduma za kusajiri line kwa alama za vidole.
Wanachokifanya ni kumwambia mpata Huduma kuwa inatakiwa atume Meseji yenye kiambatanisho cha namba za siri za mpesa kwenda 100. Wao wakiwa na uhakika kuwa Meseji haiwezi kwenda Bali itarudi ikiwa na hizo namba za siri. Hapo ndipo wanapopata mwanya wa kuiba.
Sasa nilikua nataka kujua, kutokana na wizi huu mpya, nyie mmejipangaje kuhakikisha mnawasaidia wananchi kwenye kuibiwa kwa aina hii ya wizi? Namaanisha mmeshaanza kutoa elimu kupitia njia ya Meseji ili wakitokea watu wa aina hii washughurikiwe au mnafanyaje?