Salvatory Bangi
Member
- Sep 27, 2019
- 26
- 25
Wana huduma ya ku-diactivate hizo SMS, mbona umechelewa sana ulikuwa wapi?Vodacom matangazo yenu ya biashara yamezidi sana. Kila wakati vi-message vya matangazo, mnabia sana bhana. Wenzenu Tigo angalau wamebadilika, mmeanza ninyi sasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.
Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.
Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.
Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom
UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.
Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.
UPDATE
=====
Nimeonana na waheshimiwa sana wa Customer Care pale Block 4 Mlimani City.
Cha kusikitisha ni wao kushindwa kuchukua malalamiko yangu na kuyafanyia kazi, na hii ni licha ya kuwaelewesha kuwa hili tukio nalijawahi kunitokea na hii kuwa ni mara ya kwanza.
Hawa jamaa wa Customer Care ni kama mabalozi waliopewa jukumu la kusafisha kampuni ya VODACOM hata kama inanuka kwa wizi uliodhahiri.
Kitu ambacho hawajui ni kuwa nilifanya due diligence kupitia wafanyakazi ndani ya VODACOM walionidhihirishia kuwa kuna wafanyakazi wasio waaminifu ambao wana access na personal security settings za wateja.
Na wafanyakazi hao huwa "wapiga kishenzi" fedha za wateja.
Kwa kifupi mtu wa Customer Care ameshindwa kuniconvince na maelezo yake ya upotevu wa Tshs 20,000 katika mtandao wa VODACOM.
hili ni tatzo, ht ukinunua cha 500 unaambiwa dk25 mitandao yote, ajabu ukishanunua unaambiwa dk10 mitandao yote dk15 voda kwnd voda. Kwa nn mnadanganya?!!!Sijataka kuanzisha Thread mpya, na Ku tweet.
Kwenye kifurushi cha Cheka 10,000 dk 1250 mnasema mitandao yote, nimenunu mnanipa dk 450 mitandao yote. 800 voda Voda. Huu ni wizi
Asante,, niliomba till mwaka 2017 mwezi wa tano , ikatoka till ikauzwa na walionifanyia mpango morogoro ofisi za voda, nilipofuatilia ofisini wakapiga simu wakasema till imetoka na anaitumia mtu mwingine yuko mazimbu, wakaifungia,,sasa ikawa shida kuipata kila nikienda ofisini wananiambia kesho kesho kutwa, toka mwaka huo 2017 mpaka sasa sijapata hiyo till namomba msaadaAhsanteni kwa hii PAGE. Kuna wizi sasa hivi umejitokeza kwa MAWALA WA M-PESA. Sasa sijui na wao wanajua hama lah! Jana kuna ndugu yangu kaenda kwa WAKALA kutoa pesa, akaomba namba ya WAKALA akapewa na yule WAKALA, Baada ya kuingiza Namba ya WAKALA na kufanya utaratibu wote wa kutoa pesa, jina likaja la yule WAKALA. Ndugubyangu akamuuliza WAKALA kuwa jina lako unaitwa ERICK KIMALIO? WAKALA akajibu ndiyo. Na ndo jina lake. Baada ya hapo akathibitisha kutoa pesa. Ila tu baada ya kuthibitisha jina likaja jingine na Namba ya WAKALA nyingine na siyo ya yule ERICK KIMALIO. Tumeangaika sana kuwapigia simu ila ikashindika kupata msaada. Kuna mda tulipiga simu kwa kutumia Simu yangu, Dada mmoja muhudumu wa VODACOM akatuambia tumsomee Namba ya risiti ya Muamala aliyofanya, tukamsomea akasema kuwa huo Muhamala haupo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unasubiri nini kuhamia airtel!??Voda vifurushi vyao vimeshanishinda....nina muda mfupi tu wa kuiweka kabatini. Mana haiwezekani kila siku huduma zao ni za ajabu na vifurush vinabadilika kila wakati
Airtel ninayo tayari na hiyo voda. Ila nina mpango wa kuongeza kampuni nyingine ili niiache voda imeshanishinda.Unasubiri nini kuhamia airtel!??
Ukishindwa hamia hata Ttcl na Tigo
Sent using Jamii Forums mobile app
Jaribu Tigo inavifurushi mfano 3000 unapata dakika 125 na Sms 100 na 1.5gbAirtel ninayo tayari na hiyo voda. Ila nina mpango wa kuongeza kampuni nyingine ili niiache voda imeshanishinda. Hakuna kitu ambacho kiliniuma kama juzi nimeweka ela yangu nijiunge nikiwa najua kabisa kifurushi fulani kipo, cha ajabu tafuta tafuta na wewe kifurush hakipo, vipo vifurushi vya ajabu tu. Itabidi niongeze vocha ili nipate kifurushi kingine chenye unafua lkn ndo ivyo ni aghali. Airtel sihami kwa kweli. Na voda nitaiama.
Asante sana mkuu kwa ushauriJaribu Tigo inavifurushi mfano 3000 unapata dakika 125 na Sms 100 na 1.5gb
5000 dakika 250 gb 3.5 ,sms 100 kwa wiki nzima
Voda nashindwa kuitetea sijawahi kutumia
Ttcl nayo ni bomba sana vifurushi vyake
Sent using Jamii Forums mobile app
Boresheni internet huku kwetu Kigoma Kibondo vijijini kwani mtu akinunua bando la internet huweza kufia kwenye simu kwa kukosa mtandao la sivyo tutawakimbia
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania