Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom matangazo yenu ya biashara yamezidi sana. Kila wakati vi-message vya matangazo, mnabia sana bhana. Wenzenu Tigo angalau wamebadilika, mmeanza ninyi sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wana huduma ya ku-diactivate hizo SMS, mbona umechelewa sana ulikuwa wapi?
.
Go kwenye website yao mwambie TOBI akupe hizo namba very easy
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Nilisajili namba yangu ya vodacom kwa alama za vidole na nikasajili m.pesa pia ila baada ya kutumia m.pesa kwa muda wa wiki 3 mara gafla watu wakitaka kunitumia pesa kwa m.pesa linatoka jina la mtu mwingine na wakati namba ni yangu na nimesajili mwenyewe,nimeamua laini yenyewe niitie kwenye kabati la vyombo tu maana huu ni utapeli


Sent using IPhone X
 
Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.

Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.

Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.

Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom

UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.

Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.

UPDATE
=====
Nimeonana na waheshimiwa sana wa Customer Care pale Block 4 Mlimani City.
Cha kusikitisha ni wao kushindwa kuchukua malalamiko yangu na kuyafanyia kazi, na hii ni licha ya kuwaelewesha kuwa hili tukio nalijawahi kunitokea na hii kuwa ni mara ya kwanza.

Hawa jamaa wa Customer Care ni kama mabalozi waliopewa jukumu la kusafisha kampuni ya VODACOM hata kama inanuka kwa wizi uliodhahiri.
Kitu ambacho hawajui ni kuwa nilifanya due diligence kupitia wafanyakazi ndani ya VODACOM walionidhihirishia kuwa kuna wafanyakazi wasio waaminifu ambao wana access na personal security settings za wateja.

Na wafanyakazi hao huwa "wapiga kishenzi" fedha za wateja.

Kwa kifupi mtu wa Customer Care ameshindwa kuniconvince na maelezo yake ya upotevu wa Tshs 20,000 katika mtandao wa VODACOM.
 
Takukuru ichunguze ofisi ya afya kilimanjaro



Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa kilimanjaro wanaiomba taasisi ya takukuru mkoawa kilimanjaro kuzichunguza ofisi za ras, chama cha waandishi wa habari kilimanjaro na ofisi ya afya mkoa wa kilimanjaro kwa ubadhirifu wa fedha za semina ya korona iliyofanyika moshi

Waandishi hao wanasema kuwa walialikwa kwenye semina hiyo ya mafunzo kuhusu ugonjwa korona wakiwa zaidi ya 20 bila kupata malipo yoyote pamoja na kuwa waliorodheshwa kama washiruiki wengine wote



Cha kushangaza ni kuwa taarifa zilizopatikana mjini moshi zinasema kuwa waandishi walilipwa kuwa kushiri semina hiyo ya mafunzo kuhusu ugonjwa wa korona pamoja na kuwa wakati wa ufunguzi wa semina hiyo afisa wa afya kilimanjaro bw. Jonus Mcharo aliwaambia kuwa wao wameshiriki ili kupata taarifa na ujuzi wa kuandika habari za korona kwa usahihi



Baada ya mafunzo hayo waandishi wa habari walisubiri utaratibu mwingine kuhusu nauli kama washiriki wengine walivyoahidiwa ena mbele ya waandishi wakati inaanza lakini wakaambiwa na viongozi wa waandishi mecki kuwa hakuna nauli zao waandihi wakaondoka



Taarifa za juzi baada ya uchunguzi wa kina zinaonyesha kuwa waandishi wote walioshiriki semina hiyo walilipwa posho zao sawa na washiriki wengine tena siku zote 4 ingawa wao walishiriki siku ay ufunguzi tu hata hawakupata nafasi ya kupata hotuba ya mgeni rasmi



Taarifa zinaonyesha kwa siku 4 waandishi wot wlailiopwa siku ziot 4 fedha kati ya shilingi milioni 6 na shilingi milioni 8 kutokana na idadi yao ingawa haijawekwa wazi



Tunajiuliza hapa ni kwanini waanishi wasilipwe na wao walishiriki kama wengine wakaacha shuhuli zao kama wenzao?



Jee mikoa mingine walifanyiwa hivyo hivyo kwenye semina kama hizo?

Mbona mcharo aliptoka viongozi waliwaambia waandishi wasubiri awape jibu kwani jibu la waandishi walipwe au wasilipwe nauli alienda kulichukua wapi na la nini wakati alishasema wamekujwa kuchukua ujuzi tu?

Kuna taarifa kuwa alikwenda kuchukua fedha za waandishi mapema ili wanakamati wenzake wasijue na alipokuja akasema nauli za waandishi hakuna sasa mbona aliondaka na afisa habari wa mkoa kwenda ofisini kwake? Maana inasemekana alikwenda kumkabidhi fedha za waandishi baada ya kugawana na mcharo akabaki za za kwake yeye na wanakamati wenzake mafisadi na aliporudi nje afisa habari wa mkoa ndiyo akasema hakuna nauli za waandishi na waandishi wakaondoka zao, sasa hizo walizopewa baadhi ya viongozi wa meki na waandishi ambao ni marafiki wa viongozi wa meki na afisa habari huyo zilitoka wapi?

Takukuru wapige hasena za waandishi 20 tu kwa shilingi 50,000 kwa siku yaani 200,000 kwa siku 4 ni shilingi ngapi? Mbona hawakupewa wote? Kuna taarifa kuwa malipo yalikuwa ni 80,000 kwa siku

Hii si mara kwanza kwa waandishi kufanyiwa ufisadi huu, juzi juzi pia waliambiwa wajiorodheshe ili walipwe fedha za ziara waziri mwakyembe mpaka leo hawajalipwa lakini kuna wengine inasemekana wamelipwa wakiwa viongozi wa meki pia kwanini wao tu? Kuna malalamiko mengi ya waandishi kuandikishwa na afisi ya habari mkoa wa kilimanjaro kwa ajili ya malipo ya ziara au kazi zingine lakini hawalipwi lakini wakienda mitaani wanasikia malipo yametoka kwanini na wengine wanakatwa majina yao baada ya fedha kutoka?

Hivi maafisa hawa na afisa afya kilimanjaro hawajui umuhimu wa waandishi wa habari kazi kubwa wanayofanya katiak kuripoti habari hizi zinazotolewa kila mara na serikali mpaka za viongozi wa juu kabisa?



Kwa nini wawaorodheshe waandishi kwenye orodha ya washiriki wote halafu wasilipwe na wengine walipwe? Kwanini waandishi wengine walipwe kwa siri an wengine wasiliopwe fedha zao zimeenda wapi?



Ukweli ni kuwa kuna ubadhirifu umefanyika na ofisi ya ras inajua ofisi ya afya inajua na ofisi ya meki inajua
 
I see nimeanza kuitumia voda tangu mwaka 2006,l na sijawahi kubadili namba. Ila mmeanza kuwa wasumbufu (sijui mmelewa sifa) wiki iliyopita nimemuunga mpenzi wangu kifurushi cha 10000 cha ajabu hakionekani kwake na kwangu salio mmekata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ukweli usiopingika......vodacom siku nyingi tunawaangalia tu kwenye issue ya data na vifurushi.....lakini angalau kwa kipindi hiki kigumu angalieni....baadhi ya wanafunzi wanasoma online, meetings, kazi etc... nyingi zinafanyika online ...ila data zenu zinayeyuka fasta kama mwanga wa radi.
Pia kifurushi cha university offer 2000 unapata mb 512 kweli......hii mb hata haikai kwa jinsi mnakata sana ....
Airtel, Tigo, na Halotel nanyi liangalieni hilo hila Vodacom amezidi sana.
 
Sijataka kuanzisha Thread mpya, na Ku tweet.

Kwenye kifurushi cha Cheka 10,000 dk 1250 mnasema mitandao yote, nimenunu mnanipa dk 450 mitandao yote. 800 voda Voda. Huu ni wizi
hili ni tatzo, ht ukinunua cha 500 unaambiwa dk25 mitandao yote, ajabu ukishanunua unaambiwa dk10 mitandao yote dk15 voda kwnd voda. Kwa nn mnadanganya?!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsanteni kwa hii PAGE. Kuna wizi sasa hivi umejitokeza kwa MAWALA WA M-PESA. Sasa sijui na wao wanajua hama lah! Jana kuna ndugu yangu kaenda kwa WAKALA kutoa pesa, akaomba namba ya WAKALA akapewa na yule WAKALA, Baada ya kuingiza Namba ya WAKALA na kufanya utaratibu wote wa kutoa pesa, jina likaja la yule WAKALA. Ndugubyangu akamuuliza WAKALA kuwa jina lako unaitwa ERICK KIMALIO? WAKALA akajibu ndiyo. Na ndo jina lake. Baada ya hapo akathibitisha kutoa pesa. Ila tu baada ya kuthibitisha jina likaja jingine na Namba ya WAKALA nyingine na siyo ya yule ERICK KIMALIO. Tumeangaika sana kuwapigia simu ila ikashindika kupata msaada. Kuna mda tulipiga simu kwa kutumia Simu yangu, Dada mmoja muhudumu wa VODACOM akatuambia tumsomee Namba ya risiti ya Muamala aliyofanya, tukamsomea akasema kuwa huo Muhamala haupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante,, niliomba till mwaka 2017 mwezi wa tano , ikatoka till ikauzwa na walionifanyia mpango morogoro ofisi za voda, nilipofuatilia ofisini wakapiga simu wakasema till imetoka na anaitumia mtu mwingine yuko mazimbu, wakaifungia,,sasa ikawa shida kuipata kila nikienda ofisini wananiambia kesho kesho kutwa, toka mwaka huo 2017 mpaka sasa sijapata hiyo till namomba msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Voda vifurushi vyao vimeshanishinda....nina muda mfupi tu wa kuiweka kabatini. Mana haiwezekani kila siku huduma zao ni za ajabu na vifurush vinabadilika kila wakati
 
Unasubiri nini kuhamia airtel!??

Ukishindwa hamia hata Ttcl na Tigo

Sent using Jamii Forums mobile app
Airtel ninayo tayari na hiyo voda. Ila nina mpango wa kuongeza kampuni nyingine ili niiache voda imeshanishinda.

Hakuna kitu ambacho kiliniuma kama juzi nimeweka ela yangu nijiunge nikiwa najua kabisa kifurushi fulani kipo, cha ajabu tafuta tafuta na wewe kifurush hakipo, vipo vifurushi vya ajabu tu. Itabidi niongeze vocha ili nipate kifurushi kingine chenye unafua lkn ndo ivyo ni aghali.

Airtel sihami kwa kweli. Na voda nitaiama.
 
Airtel ninayo tayari na hiyo voda. Ila nina mpango wa kuongeza kampuni nyingine ili niiache voda imeshanishinda. Hakuna kitu ambacho kiliniuma kama juzi nimeweka ela yangu nijiunge nikiwa najua kabisa kifurushi fulani kipo, cha ajabu tafuta tafuta na wewe kifurush hakipo, vipo vifurushi vya ajabu tu. Itabidi niongeze vocha ili nipate kifurushi kingine chenye unafua lkn ndo ivyo ni aghali. Airtel sihami kwa kweli. Na voda nitaiama.
Jaribu Tigo inavifurushi mfano 3000 unapata dakika 125 na Sms 100 na 1.5gb


5000 dakika 250 gb 3.5 ,sms 100 kwa wiki nzima

Voda nashindwa kuitetea sijawahi kutumia

Ttcl nayo ni bomba sana vifurushi vyake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMIYU VODACOM HUDUMA

MANAGER KANIAMBIA NIENDE NIKAONANE NA UONGOZ VODA

ALICHODAI HAWEZ KUNISAIDIA
SABABU NILIANDIKA UJUMBE KWENYE KURASA ZA VODACOM TANZANIA MESENJA

KWA HIYO NILIHARIBU SURA YA VODACOM PAMOJA NA YEYE NILIMHARIBIA
Kwa maana hiyo hatoweza vinginevyo niende uongoz wa juu

Pia tuliendelea kujibishana ama kuchat nae kwa njia ya sms kwa dakika kadhaa

Meseji chat za whatsapp nimezihifadhi kwa Google kama docs

Mwenye namba ya wakala mkuu

DAILY TRADE MARKETING aje inibox

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boresheni internet huku kwetu Kigoma Kibondo vijijini kwani mtu akinunua bando la internet huweza kufia kwenye simu kwa kukosa mtandao la sivyo tutawakimbia
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
 
Malalamiko yangu ni mengi sana, ila kwa leo nawasilisha malalamiko ya kutokupatiwa line ya wakala tangu mwaka juzi.

Mwaka juzi nilimpatia wakala wangu wa eneo vielelezo vinavyokiwa niweze kusajiliwa line ya M-MPESA lkn hadi muda huu, ninapowasilisha malalamiko yangu sijapatiwa line.
Nilijaribu kufuatilia kwa karibu nikagundua vielelezo vyangu vilitumika kusajiliwa line kwa mtu mwingine na akawa anatumia hiyo line kwa jina langu.

Malalamiko haya nimewasilisha kwa meneja anayehusika na line, na baada ya kumsumbua sana amenitumia TILL ila line bado hajanipatia na hata nikimpigia simu hapokei.

Tafadhali naomba wahusika mulifanyie hili kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vodacom nyie ni takataka kabisa nilikua nawaona wa maana sana lakini nyie ni rubish Indeed mazafanta.

Yaani nimejiunga kifurushi cha dk150 voda, dk 15 mitandao yote + 1GB, maajabu yenu nyie wahuni mmenipa dakika lakini MB 0 (zero) yaaani mmenila MB zote juu kwa juu.
Nawapigia huduma kwa wateja wananiletea story za masaa 24 watashughulikia wakati me nina shida na MB muda huu.

Nasema hivi VODACOM TANZANIA acheni uhuni na wizi maaanina zenu.

Songesha mmenipa 28,000/= kesho mapema sana naichomoa af mazoea yanakatia hapo. Yaaaani msinizoeee kabisa maanina.

Screenshot_20200426-223532.jpg
 
Back
Top Bottom