Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom mmeniboa Sana wafanyakazi wenu wanawaangusha hawapo kikazi ila kimaslahi zaidi Tatizo langu toka mwezi 5 baada ya kuwatafuta viongozi wajuu Jana ndo wanahangaika yaani nimekerekwa kweli.

Ushauri katika menu yenu ongezeni kipengele kitakacho mwezesha mteja kuripoti mwenendo mbuvu wawafanyakazi kweli mnakera,
 
Hilo lipo maana siku narusha salio ili ninunue mda wamaongezi imekatwa nawapigia wanasema ulikopa mda WA maongezi nawauliza lini.

Najibiwa hawawezi kata Kama huna Deni.
 
Vodacom mnatuibia sana kwenye M-Pesa. Unatoa pesa kidogo tu lakini makato elfu nane. Siku moja nimetoa milioni mbili kwenye akaunti yangu ya M-Pesa lakini nilichokiona sikuamini asilani. Nilikatwa elfu nane, jambo ambalo kama ningetolea ATM kwa mikupuo mitatu ningechajiwa elfu 4000 au chni ya hapo.

Kwa hili la M-Pesa mnakera sana na wizi wenu huu wa wazi wazi na msipobadilika watu wengi sana watawakimbia pale tu mtakapogundulika na watanzania walio wengi ambao kwa sasa bado hawajajua namna mnavyowapiga wazi wazi kiasi hiki
 
Kumekuwa na tahadhali kutoka mitandao ya simu hasa Vodacom (M-PESA) kwamba wakala ukimuwekea pesa mtu ambae yupo mbali hautalipwa kamisheni yako ya muamala huo. Hii inaweza kuwa sawa kwasababu za kibiashara lakini kwa mawakala hili ni tatizo kwasababu mtu anaweza kudanganya kuwa anaweka pesa kwenye simu yake kumbe anamtumia mtu wa mkoa mwingine tofauti na alipo.


Kumbuka huwezi kumwambia mteja lete simu yako hapa nione kama SMS ya muamala unaingia kwako. Mwisho wa siku hii inakuwa imekula kwako wewe wakala kwa kukosa kamisheni yako.

Nini kifanyike?

Makampuni haya ya simu tengenezeni mfumo ambao utawawezesha mawakala kupewa WARNING wakati wanaweka pesa kwa mteja kama yuko mbali simu ikutahadhalishe kwamba "mtu unaemuwekea hela yupo mbali na eneo lako hivyo hautalipwa kamisheni yako, kuendelea bonyeza labda "1" kusitisha muamala bonyeza "2". Hii itasaidia kuwapatia kamisheni zinazostahili mawakala wanaowasaidia kuwafikishia huduma karibu na wananchi.


Asante. Natumaini maoni yangu yatafanyiwa kazi.
 
Nimejiunga GB 4 kwa week ila kesho yake tu ishaisha wakati sijadowload mavitu wala sijaangalia you tube. Nimekuwa nikivumilia ila hii imezidi. Imebidi nijaribu kwingine nikanunua GB 1 kwa siku tatu, imeenda vizuri leo siku ya tatu bado zimo 140 MB.

Kwaherini nyinyi si saizi yangu.
 
Nyie Vodacom mbona mnazuia ujumbe wenye jina Tundu Lissu kutoka,mna ajenda gani ya siri. Kwa nini mnajiingiza kwenye siasa
 
Vodacom ongezeni kwenye menyu yenu ya *149*01# command ya kurudi nyuma kila hatua unayokwenda kama mitandao mingine walivyofanya kuliko mtu kucansel kila mara anapotafuta aina ya vifurushi anavyotaka. Natumaini mtafanyia kazi.[emoji853]


Sent from cupboard using mug
 
Vodacom nawaambia tuu kuwa sasa hv nna sim card ya halotel
 
Kwa nini mnafanya hivi Vodacom, kuanzia mwezi wa kumi, vifurushi vyenu havikai, mtu unanunua kifushi Cha wiki ndani ya saa au siku kimeisha wakati ujafanya chochote, kuweni na huruma kwa pesa za wenzenu, kwa nini nilipie wiki, na huruma iishe kabla, waliosomea Sheria msaada please,
 
Vodacom, hivi designer wa matangazo yenu ya sms mnazotutumia ni nani? ,mnaandika vitu vingine very nonesense hadi mnakera! kuna li sms mnalituma kila siku asubuhi limeandikwa "SHANGWE SHANGWENA" Ni nini hiki? mnakera na sms zenu za matangazo za hovyo hovyo, mnadhani wateja wenu wote ni wanafunzi wa sekondari au? nyie mnakera sana,,,nimebaki kuwa mteja wa MPESA tu kutokana na kua nafanya kazi sehemu ambayo wanatumia kampuni yenu kulipitisha miamala otherwise, i dont recomend mtu anunue sim card yenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…