TUSUA SPOTI..mchezo wa kubahatisha unao endeshwa KITAPELI.
Nasema kitapeli sababu ya kwamba mnatumia maneno ya kilaghai kwa mteja huku mkijua kabisa sivyo ilivyo huo ni wizi.
Mfano ukisema watu washindane kukimbia na mshind wa kwanza ata jishindia elfu 60 mfano alafu,asa mtu akimbie na baada ya kua wa kwanza ndio muongeze neno jipya na sheria nyingin ala mtu ajikute amekua wa kwana na asipate zawadi yoyote huo ni ulaghai ( UTAPELI ).
Maelezo ya tusua spoti yanasema.
"Unatakiwa kuchagua majibu sahihi kwa haraka kwa kila mechi 14 zilizochezwa.Utashinda kama utajibu kwa usahihi maswali 6 au 7 ya kwanza,au maswali 11,12,12 au 14 utakayopokea.kiasi cha Tsh.50,000,000 kutolewa kila siku."
Tuachane na izo million kadha ambazo mnasema mnatoa kila siku.ila tayari mmesha ahidi kua utashinda ata ukipatia majibu 6 tu ya mwazo utashinda sio utaweza kushinda ni utashinda ndivyo maelezo ya navyo sema.
Ukishiriki tu bahati nasibu hii unapata meseji nyingine inasema hivi.
"WASHINDI DROO YA SAA wa leo wenye majibu sahihi 14 watapata kiwango cha chini Tsh 50,000 na 13: Tsh10,000 na 12: Tsh2,500 & 11: Tsh 500!
Endelea kucheza ushinde zawadi kabambe!"
Yani ayo maelezo yako wazi washindi wenye majibu 14 sahihi wata pata kiwango cha chini Tsh.50,000.ya ni maana yake wote watapata maana maelezo ayajasema atapata, bali watapata ata kama wako 10.na sio chini ya elfu 50.ndivyo maelezo ya navyoeleza.
Mimi nikashiriki mara kadha na nikafanikiwa kupatia mjibu yote ya mechi 14 nikapata msg hii.
"Umefanya vizuri!
Umejibu kwa usahihi maswali 14
Kwenye spoti slip kwa tiketi namba 15.
Utaingia kwenye droo saa 10:00:00 na washindi wote waliojibu maswali 14 kukomboa zawadi ya Tsh50,000"
Maelezo ya nasema ukipatia majibu 14 sahihi unapata elfu50 na apo pia mmesema washindi wote,na sio mmoja wao wote.na sio ataweza hapana ni wamekomboa nini maana ya kukomboa yani ni kama kitu akikua chako au ulikiweka lehani sasa umekikomboa yani kimekua chako..kwa maelezo hayo nikwamba ata mkichezesha iyo droo na sijafanikiwa kupata ayo ma million tayari mimi nimekomboa Tsh50,000 kama maelezo yenu yote ya navyo sema aijalish tupo wangapi mmesema wote.
Asa nashindwa kuelewa baada ya hiyo droo naambiwa tiketi inayo fata ni bure umeshinda Tsh500 isiyo hamishika ila unaweza ichezea tiketi inayofata yani iyo Tsh500 siwez ata ichukua mana yake nimepatia mechi zote 14 na nimeambulia tiketi ya bure wakati nilihakikishiwa elfu50.naiyo tsh500 ni anastahili apatiwe yule aliye patia mechi 11 tu kwa mujibu wa maelezo yenu kuhusu mchezo huu.
Alafu cha ajabu zaidi ata iyo tiketi ya bure siwezi cheza maana mmeniwekea Tsh 425. Na tiketi ni Tsh 500. Huku kiwango cha chini kuweka ela kutoka mpesa ni Tsh1000 manayake akuna na mna yoyote naweza itumia iyo Tsh 425.
Kwaiy kwa sasa mimi nawadai Tsh50,000 kwakupatia majibu sahihi 14 kwenye spoti slip id15.
Kama mtabadiri sheria za mchezo na maelezo mbadiri ila mkishanipatia zawadi yangu niliyoshinda