Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)


Wasiliana na Skype apo boss ninachoona tatizo halipo Voda coz wao wameisha ruhusu malipo skype ni jukumu lako kuwatafuta skype sasa uhoji wamepokea pesa ila hawajatoa huduma
 
Habari,
Mbona hii visa card hairejeshi sms ya malipo baada ya kulipia kitu mtandaoni?

Alafu customer care tunawapataje?
Mnatupotezea muda sana wakati wa kutaka huduma!
 
Habari,
Mbona hii visa card hairejeshi sms ya malipo baada ya kulipia kitu mtandaoni?

Alafu customer care tunawapataje?
Mnatupotezea muda sana wakati wa kutaka huduma!
Mastercard inasumbua kwa sasa nafikiri
 
Name:
Number: Vodacom
Content:
UPO TAYARI? Kesho tuna Jambo Letu, USIKOSE
Time: 02/12/2021 10:40:14
 
Vodacom siku hizi mbili internet yenu ina shida gani....mbona iko chini kupiliza yaani inapiga mpaka 0.0kb/s kweli wakati nyie ndo mko vizuri Kwa speed.

Tatizo ni nini????
 
Kuna shida kubwa sana,
Pindi unapotaka kuongea na mtoa huduma.

Kama huamini jaribu kuwapigia ili usikie hizo ngonjera zao.
 
Mkuu mm ninashida na statement ya till yangu nimejaribu kutembelea voda shop wameniambia niwasiliane na wakala wangu mkuu ilhali simjui nimejaribu kutafuta mawasiliano naye aliye nitengenezea till amekuwa akinichenga sijui mnanisaidiaje kwa hilo
 
Habari waungwana,nataji msaada wa line yangu ya vodacom mpesa,line hii niliuziwa na mtu miaka mitatu sasa imepta ,aliniuzia nikaendelea kuitumia baada ya yeye kufunga bihashara ya huduma za kifedha,sasa aliama mkoa na sina mawasiliano yeyote nae ,sasa juz line yangu imegoma gafla kusoma,sasa nafanyaje ili niiswap wakat mm sina document yoyote ya usajil wa lin hii,naitaji msaada wenu,atanguliza shukuran
 
Naomba kuuliza menyu ya vifurushi vya chuo unabonyeza ngapi???
 
Leo nimeweka vocha za 1,000 mara tatu kwa mkupuo ilinijiunge kifurushi cha wiki 3,000 kuangalia salio nashangaa nakutana na 2,938 bila maelezo yoyote sijui hio 62 imepotelea wapi.

Nimeweka vocha data nimezima tu muda mrefu kwabla ya kuweka vocha, sajajiunga na huduma yoyote ambayo ingenikata pesa bila idhini yangu.

Kwakweli inasikitisha mtandao mkubwa kama huu kuwa na mambo ya kitapeli kiasi hiki.

Shame on you.
 
Tuwekeeni GB10 kwa TZS 10000 kwa siku 30, na sisi tumudu kununua, sio sasa hadi simba na yanga wakicheza ndio nanunua kwa siku moja, tusaidieni tuwe online masaa mengi tujifunze vingi.
 
Kwa Bongo Vodacom ndo mtandao bora kwa upande wa internet
 
Ni namna gani naweza kununua hisa za Vodacom?
Ni Bei gani? Na Minimum inapaswa kuanza na hisa ngapi?
 
Waheshimiwa naombeni msaada,nimekwangua vocha vibaya nimeshindwa kuingiza baadhi ya number,nimejaribu kupiga Customer care sipati msaada [emoji25],nafanyaje ili niitumie hii vocha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…