Wajinga ninyi kwa mwezi mzima mmekuwa mkinitumia message za TUSUAMAPENE!!Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Piga TCRA malalako utapata majibu chap kwa harakaLeo nimejiunga kifurushi cha maongezi cha Tshs.2,000/=,kwa M-PESA,Kiasi kilichokuwemo kwenye akaunti ya M-PESA ilikuwa ni Tshs.17660.09/=,Kitu cha kushangaza salio likabaki 12,946/=.Na hawajasema pesa hiyo ya juu iliyokatwa ni kwaajili ya nini.Na nikijaribu kuwasiliana na huduma kwa Wateja sipati ushirikiano,na hii si mara ya kwanza kuna siku nyingine badala ya kukata 2,000/= wao walikata 3,000/=.Vodacom mnatunyanyasa sana wateja wenu.