Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Huu ni ushauri kwa vodacom na ufanyiwe kazi. Nimekopa m pawa kisha baada ya muda nikaweka hela m pesa na nikahamishia zote m pawa. Sasa eti vidacom wanazuia kutoa hela m pawa kwa lengo la kulipia mkopo husika. Wanasema niweke hela nyingine m pesa ndipo nilipie mkopo. Haijakaa vyema.

Hapa hapo riba inaendelea kuongezeka na meseji za usumbufu kila leo lipa lipa wakati hela yangu ipo m pawa. Basi wekeni kipengele kwenye menyu zenu cha kuruhusu kukata deni ndani ya m pawa. Hadi leo mnafikiria nini?
 
hii kero kweli. kwanza wanarudnika ria Kisha wanakata Salio lako lililopo mpawa halafu wanakufungia mwezi mzima ndo ukope Tena.

kubwa kuliko ni masms Yako na kurok mama isiwe na mawasiliano wassap
 
hii kero kweli. kwanza wanarudnika ria Kisha wanakata Salio lako lililopo mpawa halafu wanakufungia mwezi mzima ndo ukope Tena.

kubwa kuliko ni masms Yako na kurok mama isiwe na mawasiliano wassap
Ujumbe uwafikie kwa kweli
 
Mgao wa share zetu kwenye vodacom inakuwaje, mbona hatupati?

Hata tukitaka kuuza tunaambiwa haziuziki sasa fedha zetu zimeganda bila ya faida yo yote.
 
Naomba kuwasilisha:

Je,kuna tatizo lolote la kiufundi katika app ya M-PESA mteja akitaka kununua KING'AMUZI cha AZAM.

Maana nimejaribu mara kadhaa hapa napata alert ya "Kwa sasa sitoweza kukunua kifurushi maana kuna hitilafu.

Naomba ufafanuzi katika enyi Vodacom.

Ahsante.
 
mateso mliyonipa leo kwa kuzima huduma ya m pesa bila taarifa, nikitoa hela yangu nitatupa line yenu. Nimeteseka sana bila kujua sababu.
 
Naomba kujua Riba ya Mkopo wa M-Pawa, naona hawa jamaa ni kama wezi.
Nimejaribu kukopa 200,000 ikiwa salio la kwenye akaunti yangu ni 8,011.00 baada ya mkopo naona 163,854.00. Maana yake ni kwamba MKOPO WA 200,000 NIMEWEKEWA 155,843/- lakini NITATAKIWA KUREJESHA 200,000/-
Wekeni wazi riba zetu.
Semeni hapa riba yenu ni ngapi?.
 
Nyie voda kwenye swala kukamilisha kwa mawaka mgewacha mawakala wakamilisha wenyewe kuliko kuweka vikazo wakati wakala akisajili kwa nida yake kwanini mkaenda Mambo lukuki Mara wakala aje tin LESEN.yanini yote hata kwenye kuSwap voda wakala bado Kuna vikao kibao Kama unataka send of Mara muone meneja na hela juu wanahitaji uswap line yako uwakala achen hizo Mambo voda
 
Vodacom laini yenye deni la miaka 4 songesha,hatuwezi kukaa meza ya majadiliano
 
Tukutane kesho Jumanne tarehe 07/03/2023 Twitter Spaces.
 
Natumia voda tangu nianze kutumia cm na kila nikijaribu mtandao mwingine nashindwa naona bora voda yangu.
 
HIVI NINYI Voda mnatuchukuliaje SISI wateja WENU?

Bando la wiki la Tshs 20,000/= mnashusha MB KILA wiki!!!
Naamini kimefika kipindi cha kuacha kununua bando..

YAANI hamjali hali ZETU kiuchumi!!

Nipeni SABABU ya kupunguza MB kwa thamani ya PESA ileile..
 
Huduma zenu siku hizi ni chenga sana hii kanda ya mwambao wa ziwa Tanganyika. Mtandao gani huu watu mnakaa hata siku mbili haupo ukiuliza unaambiwa eti mkonga wa taifa, unabaki kushangaa tu huo mkonga ni kwa voda pekee???
Mbona mitandao mingine hakuna hizi chenga na kero.
 
Ni kweli nimekuwa kigoma....ni tatizo sana sana.....pia ukipiga simu KYELA MBEYA Mtandao wa Voda una tatizo......
 
Je, ni kweli VODA tangu muuze shares zenu hazijawahi kupanda na haziuziki?
Je, ni kweli kampuni haipati faida kama inamlipa DIAMOND PLATINUMZ mamilioni kwenye matangazo hamuoni hiyo ni moja ya sababu ya kupata hasara?
Voda semeni, watu wanataka kuuza share zao hata nusu beo haziuziki, semeni ?
 
Kwa nini kwenye huduma yenu ya nipigetafu saizi hamumpi nteja nafasi ya kukopa kiasi anachotaka? Mfano mtu kapungukiwa 400 au 500 ili ajiunge kifurushi , mnalazima ajiunge kifurushi kingine kwenye menyu yenu
 
Mfano hapo unakuta labda nina 1000, nataka nikope 500 ili nijiunge kifurushi cha 1500, unakuta siwezi kukopa hiyo hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…