Kuna mawakala matapeli sana mkuu, na hii mitandao inawaamini sana. Mimi ilikwishawahi nitokea kwa huduma hiyohiyo ya Mpesa.
Siku moja "wife" kaenda safari Mwanza na mimi nikiwa kikazi Dodoma (siku hiyo najiandaa kurudi Dar), nikaingiwa kwa wakala na kumtumia laki sita na nusu. Wife akaniambia kapata, nami nikaingia katika bus kurudi Dar. Siku hiyo wife hakuitoa hela; siku inayofuata anaenda kutoa kakuta account yake ya Mpesa imefungwa. Kawapigia jamaa wa (sijui ndiyo Voda au Mpesa) wakamuambia wakala aliwapigia simu kuwa mteja aliyemuingizia hela (yaani mimi) sikumlipa hela (cash). Kwa hiyo wameona njia sahihi si kumrudishia hela wakala, bali ni kufunga account zote (yaani yangu na ya wife), ila ya wakala hawaifungi. Wakamueleza kuwa wamefanya hivi ili tumalizane na wakala kwanza, then wakala akiwapigia kuwaambia yameisha ndiyo angeweza kuitoa hiyo hela. (Mimi hadi hapo sina habari, maana sijapata cha sms wala simu).
Wife kuambiwa hivyo ndiyo akanitaarifu. Siku hiyo nilitamani nipasuke, maana sipo tena Dodoma (nipo Dar). Kosa kubwa nililofanya kwa sababu ya haraka zangu za safari (ambalo nawashauri watumiaji wa hizi huduma kutofanya) ni kutosign ile form ya wakala kuonesha kuwa nimefanya muamala. Na hili nililiona tamu yake pale nilipomtuma "aliyekua mwenyeji wangu na ambaye alinisindikiza siku nasafiri na kushuhudia nikitoa fedha" huko Dodoma akaresolve tatizo kwa wakala. Wakala aliruka kuwa hakupokea fedha na ndiyo maana mimi sikusign fomu yake. Jamaa akajiondokea na kunipa taarifa. Hiyo siku siisahau. Ilikua saa saba mchana, nikaaga kazini. Nikawahi Ubungo (ndani ya Mohamed Trans hadi Dodoma). Niligundua kosa nililofanya la kutosign, lakini nilitaka nimuadabishe huyu wakala.
Usiku nikafika Dodoma. Asubuhi nikawatafuta jamaa (Polisi) watatu nikawaeleza kila kitu. Nikamalizana nao. Mida ya saa tano asubuhi lile eneo la stendi ya mabasi ya mikoani la Dodoma lilikuwa kama kuna "Osama" amewekwa target. Mimi nipo kwa mbaaaali nacheki movie...defender ya polisi imejaa wazee ilipiga vumbi, jamaa wakavamia kibanda cha mshikaji (juu juu wakambeba bila kueleza chochote hadi kituoni). Dakika chache mimi huyo nimeingia. Jamaa alivyoniona tu akashtuka, kumbe polisi mmoja akamshtukia kuwa jamaa keshajua kosa lake; akampa kibao (kichapo kikaanza bila kuongea neno). Kama dakika kumi hivi kuachiwa ajieleze (baada ya kuulizwa huyu unamfahamu), jamaa akasema "nisameheni, narudisha hela yake". Akawapigia simu watu wake, wakaja wakajichanga, nikapewa saba na nusu, jamaa sikutaka hata kujua watamfanya nini, nikawaacha.
In monetary terms, nilipoteza kama laki tatu. Ila niliamini nimempa fundisho ambalo hatorudia tena.