Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Wazo lako ni zuri sana.

Kwa pesa kuanzia 100,000 wangefanya 1 hour kabla hazijatolewa.
Hii upande mmoja unaweza ona nzuri ila inapotokea dharula haitafaa.Cha muhimu ni kufanya muamala kwa umakini
 
Habari kenethedmund tunapenda kukukumbusha kuhakiki jina la mpokeaji kabla hujathibitisha kutuma pesa ili kuepukana na makosa yanayoweza kujitokeza. Ahsante

Ikiwa wewe ni memaji wa vodacom hujatoa suluhisho sahihi

Inatoke wakati mwingine mtandao wenu ukiwa chini mtu unafanya muamala meseji inakuja baada ya robo saa au nusu saa meja ameshakata tamaa na kuondoka pengine ana safari.

Jee kati ya wakala au mteja huoni hapo kuna atakaepata hasara? Na kinachowazuia nyie kuonesha jina la anaetumiwa fedha kabla ya wakala kuruhusu muamala kufanyika ni nini. Mbona unapotuma toka kwenye akaunti yako ya m-pesa (sio wakala) kwenda kwa mwingine unaarifiwa kabisa unatuma fedha kwa fulani?

Inashindikana nini huduma hiyo hiyo kufanyika kwa sisi wakala? Mbona air tel money wanakujulisha kwanza kuwa muamala unaoufanya (kwa kutuma) unaenda kwa fulani. Hii inamsaidia sana wakala kwani pamoja na namba ya simu bado atahakikishiwa na jina la anaepokea kabla wakala hajaruhusu muamala huo.

Uelewe mteja anakuletea no. ya simu na ankujulisha jina la mpokeaji. Sasa nyie jina mnaonyesha baada ya muamala kufanyika. Lifanyieni kazi hili na simu za mazuio ya miamala zitapungua sana ofisini kwenu.
 
Last edited by a moderator:
Pendekezo lako ni zuri sana mkuu
 
Hii upande mmoja unaweza ona nzuri ila inapotokea dharula haitafaa.Cha muhimu ni kufanya muamala kwa umakini

Umeona mbali sana aisee

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hii upande mmoja unaweza ona nzuri ila inapotokea dharula haitafaa.Cha muhimu ni kufanya muamala kwa umakini

Mkuu jua kuwa sisi sio malaika ni binadamu tu so makosa yapo. Wazo la dk kumi ni bora
 
Habari kenethedmund tunapenda kukukumbusha kuhakiki jina la mpokeaji kabla hujathibitisha kutuma pesa ili kuepukana na makosa yanayoweza kujitokeza. Ahsante

kuna wakati inarudi namba tupu bila jina la mhusika sijui tatizo linakuwaga nini? mimi mwenyewe nimeulizwa mara kibao na jamaa zangu wanaonitumia hela kwamba sijasajili line yangu.

chukueni wazo hilo hapo juu mlifanyie kazi. msifanye biashara ya kukomoa wateja wenu kisa wamekosea namba ya mtumiwa.!!
 
Last edited by a moderator:
Hapo uzembe unahusu. unakuwa unakimbizwa na nani hadi utume pesa kusikostahili?

Nadhani vod hii idiwape presha. ni wakati sasa watz kuanza kuwa serious na mambo yenu. fuatilia details to the last dot, utaepuka usumbufu mwingi
 
Mi nina mambo ma3 na hawa M PESA. Kwanza ntandao wenu wa MPesa unasumbua sna. Mara ooh huduma ya M PESA kwa ssa haipatikani! Mbona wenzenu Tigo hwana upuuzi huo!!? Kama kukiwa na matatizo ya mtandao kwa tiGO ni mara chache.

2. Ni kwa nini wakala asione jina la mteja kabla hajaweka password kurusu mhamala ufanyike!!!? Na akimaliza mhamala kwanini asioneshwe notification kwenye cm yake kwamba hela imeingia kwa mteja flani kabla ya meseji yenyewe ambayo nayo mnaichelewesha na kutusababishia hasara!?

3. Na kwa nini huduma kwa wateja ya voda ni mbovu hivi!!? Unapiga 15000 unapigiwa manyimbo mpaka dk 10 hadi 15! Na eti mna namba ya huduma kwa wateja 15366 ambayo ukipiga unakatwa sh 100 hata kama hujasikilizwa!!?

This is not fair. Tangu lini huduma jwa wateja ikalipiwa???
NB. Mi binafsi na wengine ninaoweza kuwa influece tulishaacha kuweka pesa kwenye MPESA. Na wateja tunawashauri watumie tigo kwa uhakika zaidi. Jirekebisheni bhana.
 
Vodacom Tanzania kwanini mmepandisha viwango vya makato kimya kimya??

Mtu unashida na pesa unamwambia mtu nitumie mf. 46,500/= ili upate kutoa 45,000/= kamili. Lakini cha ajabu makato yanazidi 1,500/= ambayo mmeianisha katika majarida ya viwango vya makato. Kama mmebadilisja si mtangaze ama muedit majarida ya makato??
 
Last edited by a moderator:
Habari kenethedmund tunapenda kukukumbusha kuhakiki jina la mpokeaji kabla hujathibitisha kutuma pesa ili kuepukana na makosa yanayoweza kujitokeza. Ahsante

habari Vodacom Tanzania asanteni sana kwa kuwachunia wateja wenu mbali na malalamiko wanayotoa kila siku.. mtandao wenuumekuwa wa kulalamikiwa kila siku kwa sababu ambazo siwezi kuzitaja ikiwa ni pamoja na kupandisha gharama zisuzoeleka.. pamoja na huduma kwa mteja kulipiwa.

kweli mnajitahidi sana kuwaibia wateja.. hongereni jwa hilo..

msipofanyia kazi maoni ya wateja wenu ipo siku mtayaona tu matokeo.. asanteni sana..
 
Last edited by a moderator:
Hivi kumbe vodacom wapo humu na wanaona malalamiko kila siku wananyamaza. Tunajua mnajaribu kulipa hasara mnazopata kwa kuibiwa MPESA, maana mnaibiwa sana. Lkn waoneeni huruma wateja wenu, punguzeni wizi
 
Vodacom kuweni na Huruma kwa wateja wenu,makato yenu yanatuumiza mno
 
Wazo lako ni zuri sana.

Kwa pesa kuanzia 100,000 wangefanya 1 hour kabla hazijatolewa.
backwardness idea! hii naifananisha na mawazo yanayotokea kwa watz wengi pale inapotokea ajali barabaran bas soln ni kuweka matuta. tafakari
 
Habari bahati, tumekutumia PM kwa msaada zaidi. Ahsante
 
Last edited by a moderator:

Habari Gefu, baada ya uchunguzi ni kwamba namba uliyotupatia kwa sasa inamilikiiwa na mteja XXXXX tangu 2014-06-23 saa 11 dakika 34 jioni ambapo hapo kabla mmiliki wa namba hii uliyemtaja hakuitumia kwa zaidi ya siku 90 hivyo ilifutwa kulingana na sera kisha kurudishwa tena sokoni kama laini (kadi) mpya.

Namba hii ilifutwa akaunti ya M-Pesa ikiwa na 8696.00 Tshs ambapo mteja atatakiwa kufika Vodashop kujaza fomu kama tulivyofahamishana katika jibu letu la awali. Ahsante sana
 
Last edited by a moderator:

...asante kwa mrejesho, namba hii bado tunaitumia na ipo kwenye taarifa zetu nyeti na muhimu, mara ya mwisho ametumiwa fedha kiasi cha Tzs 150,000/= na huyo mteja wenu kaulizwa wewe ni fulani akakubali wakati anajua si yeye. so akatuibia fedha hiyo, nitawasilisha malalamiko yangu kwa maandishi TCRA....
 

Go on mkuu
 
Mkuu lete namba nichange pesa mimi shahidi namba moja tutakuwa wote kwa pilato maana jamaa anatumia namba yangu tangu May,2014, hii namba nimeitumia kuanzia March, 2005 hawana haya nimeisajili ati na yeye kasajiliwa!!!! nilishangaa ukiiweka inasoma VODACOM ila haitoi ishara yoyote kujaribu kutuma pesa ikatoka jina jingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…