kenethedmund
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 347
- 89
Kuna tatizo kubwa ambalo ni la hatari kwa Mfumo mzima wa Mpesa, Unatuma fedha kwa bahati mbaya ile hela inaenda kwa mtu mwingine ambae sio mlengwa, na unapopiga simu kwa huduma kwa wateja namba 15000 ambayo unasikilizishwa mziki kwa dakika 10 ndio wanakuhudumia kiasi cha kwamba unakuta ile hela imeshatolewa na huyo mteja ambaye sio muaminifu na matokeo yake unaambiwa endelea kutupigia atakapoweka pesa ndio tutamkata. Fikiria umetuma laki tano alafu inaenda kwa mtu ambae kwa mwezi ela inayowekwa kwenye simu yake aizidi elfu hamsini lini utapata hiyo ela?
Pendekezo ni bora wangeweka kiwango kuanzia laki moja na kuendelea mtu akitumiwa hiyo pesa asiweze kutoa mpaka either dakika 10 au 15 ziwe zimepita ili kuruhusu mtumaji kuweza kuwasiliana na huduma kwa wateja kusitisha muamala endapo alituma hio pesa kimakosa waweze kumsaidia na kuzuia huo muamala usifanyike.
Naomba tujadili