Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hivi TCRA wanafanya nini??? Mitandao yote ni wezi tu, TCRA walipaswa wafanye usimamizi wa uhakika ili kuwalinda watumiaji na adhabu kali zitolewe kwa mitandao inayowaibia wateja.
 
Hivi TCRA wanafanya nini??? Mitandao yote ni wezi tu, TCRA walipaswa wafanye usimamizi wa uhakika ili kuwalinda watumiaji na adhabu kali zitolewe kwa mitandao inayowaibia wateja.
Kwani wamewahi fanya nini hata ushangae haya??!!!
 
Hata 0713, 0655... mkuu ni hao hao juzi wamenitenda nimejiunga na xtrem kuongea dk 1 simu ikakata nikahisi labda kuna kitu nimekosea, nikajiunga tena ni yale yale sasa sijui tufanye nini turudishieni TTCL yetu ya mezani tuzibebe ktk mifuko ya rambo tutembee nazo maana ni bora kuliko huu uchafu unaoitwa 075... na 071...
 
Mim natumia mtandao wa vodacom na sijawah kuwakopa ila juzi nimeweka vocha ya shiling elf 2,wakakata elfu moja na simu yangu huwa naitumia mim peke yangu…hapo ndipo nilipo amin voda ni wezi tena wizi uliovuka mipaka!!!
 
wote wezi ila tigo na airtel na zantel wanaongoza unaambiwa kifurushi cha dakika 200 lakini kumbe dk 100 unatakiwa uongee
 

Hiyo ni kweli kabisa mdau, Vodacom wana matatizo sana nadhani kuliko mitandao mingine, my wife wangu anatumia mtandao huo, tatizo alilokumbana nalo kila mara ni kwamba akiweka pesa hata kama hajapiga ile pesa inakatwa taratibu mpaka inaisha.

Ameshawasiliana na wahusika kwa muda mrefu bila mafanikio. Nilichofanya, kwa vile hiyo namba yake inajulikana sana kwa ndgu na marafiki zake wengi, nilimnunulia simu nyingine yenye line 2. ya Voda ni ya kupokelea tu simu na kutumia huduma ya M-Pesa, hiyo ya mtandao mwingine anaitumia kwa kuweka air time na kupiga bila usumbufu wowote.

Voda bado sana!
 
mitandao yote ina kero za msimu. Leo voda baada ya muda watahamia tigo mara airtel.
hiyo ni kwel. soko la mawasiliano hapa bongo ni 'oligopoly', yani soko linakuwa na wauzaji wachache, kila mmoja yupo 'masikio juu' kusikia mwenzake atafanya nini, na ndo maana mitandao yote inafika kipindi bei zinakuwa sawa.

ila kuna wakati mbaya zaidi kwenye aina hii ya soko; ni pale wauzaji wanapoamua ku-form collussion (kama kuungana vile) ili kutengeneza bei. angalia hata sasa vifurushi vya tigo na voda vinafanana, na vilibadilika kwa karibu wakati mmoja. tabia nyingine ya aina hii ya soko ni matendo ya muuzaji mmoja yanapobadili muelekeo wa soko. huwa wanasubiri muuzaji mkubwa (mf. voda) au mwenye ushawishi mkubwa kwa kundi fulani (mf. tigo) abadili bei ndipo wafuate. kwa hiyo kwa jinsi yoyote ile bei lazima zitafanana.
 
Hivi TCRA wanafanya nini??? Mitandao yote ni wezi tu, TCRA walipaswa wafanye usimamizi wa uhakika ili kuwalinda watumiaji na adhabu kali zitolewe kwa mitandao inayowaibia wateja.

Usishangae kuona wamepofushwa macho na kuzibwa masikio kwa kipande cha rupia. Adhabu niliyo wapa hawa vodacom kufuatia wizi huu mimi nimeitupa line yao.
 

Habari Mlengo wa Kati, tafadhali tunaomba namba ya simu PM kwa mawasiliano zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Habari Ngorunde tumekutumia PM tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Bila kusahau... WAMEPANDISHA VIWANGO VYA MAKATO YA MPESA KIMYA KIMYA....
 
Kwa sasa hivi voda na Airtel ni janga. Mtandao ambao una afadhali ni Tigo Tigo. Voda kwanza haipatikani maeneo mengi halafu ni weak.
 

hawa jamaa ni wezi sana jumapili nilinunua airtime 500 via nmb mobile, nikaletewa ujumbe kabisa nimepokea sh 500 kutoka nmb ile najiunga na cheka zogo naambiwa sina salio, j4 nime weka buku nimejiunga na kifurush cha jelo cha ajabu jelo ilobaki ikaliwa from no where, jana nime kopa nipige tafu ya 900 ile najiunga na cheka bombastik naambiwa sina salio na ile salio walilo nikopesha likapotea kusiko julikana, piga customer care simu inaita tu bila kupokelewa...kuanzia jana nime iteketeza na sina mpango nao hawa wahuni wa vodacom majizi makubwa kama ccm.
 
Airtel wana afadhari amieni huku, Tigo na vodacom kweli kabisa kuna shida kubwa....full wizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…