Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ha Ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaah, bora hata mmeshitukia hawa wezi yaani mi staki kuwasikia
 

Unajua hakuna nchi yenye mijitu mijuha na mijinga kama Tanzania? Kwanini? Ukiyaibia yanasema ''unaboa'', ukiyatukana yanasema ''unaboa'' ukiwa kiongozi dhaifu kama Kikwete yanasema ''unaboa'' yaani kila jambo baya unaloyafanyia hayachukui hatua yoyote bali yanabaki kusema ''unaboa''..... Mnajua maana ya kuboa?
 
Haya majitu kila siku yanalalamikiwa lakini hayasikii kama serikali ya ccm.

Huwa sipendi kununua vocha Za kukwangua zaidi ya kutumia mpesa. Ukinunua airtime Leo kwa mpesa inabidi usubiri mpaka Baada ya siku tatu au nne ndo inaingia ktk simu yako.

Tutahama tu, just wait coz it's the matter of time.

Mi Navumilia mpaka December 31, then baada ya hapo voda itakuwa ebola kwangu.
Hata muda huu tu mpesa ni Majanga.
 
Haisaidii kuwasiliana na mmoja mmoja jirekebisheni mnatia aibu sana Vodacom Tanzania huduma zenu bado za kizamani na kiujanja ujanja


Tunaimarisha Chama, umesahau kuwa tunatafuta ushindi wa kishindo mwakani
 
M-PESA tayari inajaribu kununua muda wa maongezi.
21:06 tarehe 15 Aug, 2014
 
Poleni meyalinikuta makubwa nihivi juzi tu,nilikuwa hotel flani hivi Mwanza kidune nikala nikanywa nikijua ntatoa mpunga nmb to m-pesa,bill ikaja nikahamisha mzigo sasa hapo ndipo nilipovuja jasho kidume,Pesa imetoka bank kwenye m-pesa haijaingia ilikuwa saa1 jioni mpaka nikakopa kwa manage kwakuwa tu yunafahamiana nikaondoka Pesa imekuja kuingia keshoyake jioni ,nikiwapigia hawapokei mara wanapokea wanakula salio yaani nitaabu tupu,tangu jana nimeitupa kabisaaa wanikome Pesa zangu wanitese?

Manangina alikuwa akini text sms inakaa mpaka Siku nzima ndo niipate sijui nikusudi au?.
 

Shida sio oligopolism, ila tatizo ni regulatory framework ya serikali kupitia TCRA. Hapo kuna mchezo mchafu utakuwa unachezwa
 
Habari Mlengo wa Kati, tafadhali tunaomba namba ya simu PM kwa mawasiliano zaidi.

Mnaudhi sana voda mi kila siku nawapigia tangu mwezi wa kwanza nawaambia line yangu inagoma kwenye modem ila line nyingne ya voda inakubali, mnaniambia mtanipigia, leo nimewafuta mlimani city mnanilazimisha kununua line mpya wakati error code ipo kwanini hamshughulikii, hovyo nafikiria kuwahama
 
Vodacom wanakera, kuna hii habari ya caller tone huwa sitaki hata kuisikia lakini ya kwanza nikaona message ikinijulisha nimekatwa kiasi fulani cha pesa kwa huduma hiyo nikapiga simu customer care nikakoloma wakanitoa, nimekaa tena kama miezi 3 nikapata message ya kukatwa pesa kwa huduma hiyohiyo nikawapigia tena wakanitoa.

Sasa nimetafuta line nyingine ambayo nawazoesha jamaa na ndugu kwa kuitumia kuwapigia ikiwa popular tu, Vodacom kwa heri.
 
Halafu wewe VODACOM TANZANIA wewe! Acheni njaa hizo kila siku nakuona watu wakilalamika hapa unajipitisha na kuwaita Pm.

Kiukweli nyie ni wezi na mna njaa njaa za ajabu ajabu. Huwa nanunua muda wa maongezi Mpesa najiunga kifurushi cha wiki kikiisha watakata na hela yangu iliyobaki ikiisha ndipo wanajitumisha kimeseji chao eti "ndugu mteja kufurushi chako..... kimekwisha."

Kwanini kifurushi kikiisha msitoe notification ili mtu atumie salio lililobaki kununua kingine!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…