Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)


Mkuu hilo limenikuta. Nilijiunga Cheka Zogo ya 495 huku niliweka 1000. Kucheki salio lililobaki ni 0. Nilikasirika sana. Vodacom wanakera sana. Wako weak sana. Najiandaa kuachana nao ama kama vip ibaki kwaajili ya kupokea tu.
 
Nahisi siku hizi humu watoto wamekuwa wengi sasa kama vodacom wenyewe wapo humu kujibu hoja bado mnaendelea kutukana maana yake ni nini??

Weka hoja yako vizuri wao wanajibu sasa kama matusi tuuu watajibu nn?

Kuna vitu vingi vya kujifunza mfano me nilikuwa nimejiunga na nyimbo kama nane hivi nikisikia kwa rafiki yangu nabonyeza nyota kumbe zote nalipia nikawa nakatwa hela kwenda vodashop zao wakanisaidia kuziondoa zote
Tujifunzeeeeeee sio matusiiiiiii
 
Nani katukana hapo? Hoja zote zilizowekwa hapo juu zina mashiko,usijone bora kuliko wenzako acha dharau kwa wenzako.
 
voda ni wezi sana na ukiweka hela pesa inapungua taratibu mpaka inaisha bila hata kipiga cm au kutuma msg
 
Hakika nakubaliana
nawewe mitandao yote majanga hakuna wenye nafuu hata mmoja si tigo wala
zantel au airtel na yote hii nikutokana na udhaifu wa serikali ya
ccm.

ahaaaaa! kumbe shida ni gharama basi turudi kwenye mtandao wetu wa zamani wa kutuma barua. conclusion..
 
Mkuu hilo limenikuta.
Nilijiunga Cheka Zogo ya 495 huku niliweka 1000. Kucheki salio
lililobaki ni 0. Nilikasirika sana. Vodacom wanakera sana. Wako weak
sana. Najiandaa kuachana nao ama kama vip ibaki kwaajili ya kupokea
tu.

Hamia Airtel.
 
Mkuu nipo Airtel tangu
2005 wakati huo Celtel ya kwanza then ya pili then Zain mpaka sasa. Hata
namba sijabadili mpaka leo.

du kumbe! mi nimehamia airtel juzi baada ya voda kuniboa tena line ya voda ikipotea sihangaiki kuitafuta.
 
Voda ni umbwa kabisa yan tunaibiwa sana na hii mitandao ya simu aisee
 
Nadhani wewe upo kibiashara zaidi kuponda voda waje huko tigo ila kiukweli tigo nao ni magumashi km hao voda tu
 
Hii tabia inakera sana, eti 399 dk4 badala ya 10, 499 unapewa dk 8 badala y 15?, 649 dk 14, awali zilikuwa dk 20, wakaendelea kunyofoa moja moja mpaka zimefika hizo 14?

Kibaya zaidi, leo nlikuwa na sh. 500 nikasema ngoja ninunue hizo dk 8 eti wananitumia sms salio halitoshi! Hivi walitaka niwe na sh.ngapi ndo waniunganishe?
Huu ni wizi!!
 
Hahahahaha labda uweke buku unaambiwa vodacom kazi ni kwakooooooo
 
Si mhame, kwani mmepigiliwa misumari huko!? kila siku threads zaidi ya 2 khs Vodacom zinafunguliwa, hameni, wajue wamepoteza wateja for real wajirekebishe.

Mwezi wa 6 niliweka bundle ya internet ya mwezi, siku 2 mbele naambiwa sina bundle, zaidi ya mwezi sasa line ipo pembeni inapigwa vumbi.
 
Hata tigo the same! kila siku wanareduce min kabang zao nadhan gharama za sim zimepanda
 
mkuu kichekesho kingine mtu cm iko hewan ila ukimpigia unaambiwa haipatikan siku nzima, katikati ya mazungumzo mara wamekatika, hawajamaa hawana tofaut na chama cha miaka ya sabini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…