Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Menime toa pesa nmb tangu saa4mpaka now bilabila nanadaiwa hapa sijui nifanyeje
 
Ndo maana wakakuambia KAZI NI KWAKO. Uhame usihame KAZI NI KWAKO. Uweke vocha ya 7200 au 500 KAZI NI KWAKO. Kwakifupi kila kitu kwa Voda KAZI NI KWAKO.
 

Hamimi ninoma
 
Pole sana mkuu ila kwa upande wangu mtandao wa TIGO ndo una huduma mbovu za internet nchini Tanzania.....haipatikani Mara kwa Mara na speed ni ndogo sana.

Hii inategemeana na eneo maana rafiki yangu nyumbani kwake tigo ndo the best
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ukijiunga na kifurushi cha Tsh 495 dakika 30 cha ajabu ukitumia dakika 1 na sekunde 1 kisha ukiangalia salio la dakika na sekunde wanakuambia umetumia dakika 2 yaani umebakiza dakika 28, vivyo hivyo ata vifurushi vingine vya Tsh 250, Tsh 645, Tsh 995, Vodacom Tanzania WIZI MTUPU.
 
Ni kweli...na mimi kinachoniboa kuliko pote ni vifurushi vya data. Tofauti na Airtel (ambao wanakutaarifu kifurushi kikiisha), voda haupati alert yeyote na inaanaza kutafuna airtime....kuna kipindi namaliza hadi elfu hamsini kwa siku
..ingawa nalipiwa na kampuni lakini inaniuma sana...wasiporekebisha hii lazima nihame....TCRA liangilieni hilo pia....huo ni wizi
 
Tcra wamewekwa kunako mfuko wataongea nn sasa
 
Tatizo naloliona mm malalamiko mengi tunayoyatoa kupitia forums mbalimbali ikiwemo jf ni kama huwa tunajifurahisha tu hakuna hatua zozote zinazochukuliwaga,hata yale makongamano ya ubungo plaza ya katiba,albino and the like sidhan kama kuna chombo kinachotoa the way forward nadhan kuna haja ya kuanza ku act kimya kimya kama mkuu hapo juu alivyosema ana miaka miwili, na mengineyo.
 
Mm sku hizi sieki pesa mtandao wowote washaanza kuwa siwaminifu watakuja mpaka m pesa sasa kuiba
 
yaani mkuu unavyosema ni kweli kabisa ,mimi nashangaa kwanini wasifanye hivyo ujanja gani uwo,tambua watu wasemavyo ujanja ndio mwanzo wa wizi! Ndio hivyo wamefika hatua ya kuwaibia watu sasa
 
unajua kuna sababu mbili hivi kwanza cc wananchi hatujui wapi pa kulalamikia hata kama ukienda tcra wale watafika hapo ofc za voda watahoji ,voda watachukua fungu waliloibia watu kama milion 300 watawapa milion 50 yalivyo majinga yanaondoka nyuma mzungu anawacheka cc tunaumia!

Pili watumiaji tuna ile kudharau husema kama wameiba tsh mbili tu mbona ndogo sasa fikiri kwa watu milioni 10 ni kiasi gani utakuta its lot of money
 
Habari dotnet tafadhali wasiliana nasi kwa msaada zaidi. Pole sana
 
Last edited by a moderator:
Habari Crimea, tafadhali tunaomba utufahamishe SMS hizo zinatumwa kutoka namba gani. Tuma taarifa PM kwa msaada zaidi, pole sana.
 
Nimekua nanyi toka 2007. Lakini sasa nimefika point of no return. Mmeniibia vya kutosha.

Nimepiga simu mara nyingi kulalamikia upotevu wa pesa zangu kinyemela,kila siku natumiwa sms kwamba tatizo langu limeripotiwa,mara piga baada ya masaa 3 ili system iandike matumizi yako,nikipiga naambiwa vile vile.

Vodacom ya sasa imekua inanyang'anya watu pesa zao kwa nguvu,ukiacha pesa kwenye simu kesho yake huikuti na huambiwi ilipoenda. Juzi,jana na leo mmeniibia pesa zangu bila maelezo. Kwa kua siwezi kuwapeleka mahakamani,ngoja niwahame.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…