Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)


inawezekana wewe umepoozwa tu mimi wameniibia tshs 30337 na 600mb eti wananiambia zimetumika kwenye data ndani ya saa tatu na ni kwenye simu..voda ni waizi..na ninahamia airtel..
 
Hili jambo lilinitoke hata mimi majuzi tuu, kila nikitaka kujiunga kifurusha ina kataa lakini salio lina katwa hadi likaisha. nili kerwa sana siku hiyo lakini niliwapigia tuka yamaliza na customer care.

Vodacom ni wasikivu sana.

voda ni waizi majambazi kama ccm, tarehe 28.12.2013 wameniibia 30337 na kifurushi cha 600mb ndani ya saa tatu na ni kwenye simu, nimefatilia mpaka nimechoka nimeamua kuwa hama tu...
 
Airtel ya tosha, nyingine za nini? buku tu unapewa dkk 40 za kupiga mitandao yote bila kusahau internet na sms
 
Siwezi kubisha. Utamu wa fweza umewakolea wahudumu wa mtandao huu! Dawa ni kuhama tu.
 
Airtel ya tosha, nyingine za nini? buku tu unapewa dkk 40 za kupiga mitandao yote bila kusahau internet na sms

Mkuu nijulishe kuhusu internet unapewa mb ngapi?
 
Uzembe wako mwenyewe afu wawalaumu voda, wakuibie wewe una nini cha kuibiwa
 
nachokiona voda hawana cha kupoteza kutoka kwa mteja mmojammoja wa eneo lenye ushindani km dar ambako watu wanabadilisha line kila kukicha.

wateja wao wengi ni makampuni 'corporates' na wana hazina ya wateja wengi wa muda mrefu 'royal' hasa mikoani.huko ndo wanapiga hela ndefu na ya uhakika.
 
vodacom ni wezi sana mi nilishawafata hadi oficini kwao ubungo na kuwatishia kuwapeleka Tume ya mawasiliano. yaani wanaiba sana hela zilizo kwenye mpesa, wakikutumia hata msg ya matangazo yao ukiangalia balance kwenye mpsea utakuta wamekuchagi
 
Heheheee... JF ni balaa... Customer Care kasepa.. Waja leo warudi leo..
 

Niliona wametoa tangazo kule twitter wakisema UKIWA NA SALIO LAKO HAKIKISHA UMEZIMA INTERNET KWANZA AU USWITCH OFF NDO UNUNUE KIFURUSHI, Jaribu hiyo, ila mimi Niko Airtel Mkuu,


Halafu Nyie Watumiaj wa Voda Threads zenu zmezd humu kulalamika kila uchao harafu hamchukui action Hameni Bwana!!
 
wadau vodacom sasa hivi nao ni wanasiasa,nimenunua umeme kwa m-pesa tangu saa mbili mpaka sahvi wamechukua pesa yangu hawajanitumia namba zangu za umeme nawapigia wananipa majibu kama ya mawaziri mizigo,,,ah tanzania kiboko.
 
Mkuu nijulishe kuhusu internet unapewa mb ngapi?

Mb 300 kama sijakosea, ila kuna cha watumiaji wa kawaida na wenye kipato cha kawaida kama sisi 3000 unapata Dk 100 kwenda mitandao yote, Mb 400 utumie ndani ya wiki
 
Pole sana ndugu, kunakipindi walikula hela yangu na umeme sikupata kabisa. Tangu kipindi hicho nimeshapata somo.
 
Jana nilipigwa buki tatu kwa dizaini hiyo na mtandao nimeshahama,nipo baba lao
 

Mbona mitandao mingine haiwi hivo
 
Mimi nilihama huko siku mingi sana baada ya kuona mitandao mingine inanafuu zaidi, na washkaji kibao wameshaga hama pia baada ya kugundua wanakatwa hela bila kuelewa wametumiaje
 
TCRA wana mtindo wa kukalia malalmiko ikipita wiki mbili hawakujibu wakilisha malalamiko kwenye tume yaa ushindani ofisi zao ziko ubungo

Vodacom wameiweka serikali hii mfukoni. Hakuna cha wizara ya mawasiliano wala hiyo TCRA wala Polisi, wote wamevimbiwa sumu waliyokula - "Rushwa".

Haiwezekani nchi nzima walalamike na wahuni hawa wajifanye hawasikii!
Nyerere alisema ukishapokea rushwa unageuka mtumwa, na sasa tumeyaona. Haya ni matokeo ya viongozi kuhongwa hisa na kuwa "wadau" wa makampuni ya kitapeli kama hawa Vodacom na Tigo.

Washenzi hawa wanafanya dhambi ambazo wangezifanyia huko wanakotoka wangeaibika hata wakose pa kuficha sura zao.

Ni wajibu wa TCRA kuhakikisha usalama wa wananchi dhidi ya wizi unaofanywa na makampuni yaliyosajiliwa nayo.
Wanawafumbia macho tu kwa sababu wao ni wanufaika wa hujuma hizo.

Huu wizi ulianza kwa hela ndogondogo kama sh. 20/=, 50,100 na sasa hata 10000/=! Serikali "sikivu" bado imelala kitandani kimoja kimahaba na wahalifu hawa. Hawa hawana tofauti na vibaka wa mitaani ni lazima washughulikiwe na serikali au sisi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…