Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,741
Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.
Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.
Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.
Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom
UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.
Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.
inawezekana wewe umepoozwa tu mimi wameniibia tshs 30337 na 600mb eti wananiambia zimetumika kwenye data ndani ya saa tatu na ni kwenye simu..voda ni waizi..na ninahamia airtel..