Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Kuna kitu nadhani watu wengi wanaolalamika kuwa wanaibiwa mnakosea. Kama unatumia smartphone na hujajiunga na bando la internet ni lazima pesa yako itaendelea kuliwa taratibu hadi iishe. Cha msingi kama wewe hutumii inernet nenda kwenye mobile network then iweke off! Otherwise applications ambazo zinafanyakazi katika background zitamaliza pesa yote.

Subiri nimeweka 1000 najiunga na chekabomba wanasema salio halitoshi ukicheki tena salio 897napont ukijiunga lands ya 800 haitoshi salio tena 756 napoint mpaka kero kasheshe wapigie watapokea kesho yake hawafai
 
Kuna vijana wanafanya kazi kwenye makampuni ya Simu PCCB inawahusu sana. Wamejenga Majumba mazuri tu Goba na Mbezi juu wakati Mwaka jana tu walikua wakizunguka na bahasha za Khaki maofisini.

Mfano katika wateja 4mil, ye akaamua kila wiki kuchukua wateja laki 5 tu kwa kuwala Tshs 100/- each tayari ana 50Mil

Nikweli mkuu
 
Mnamsaidiaje mtu alie vijini mfano malinyi hakuna huduma za voda shop! nimeibiwa simu nimeomba msaada kua nikombali naomba muiblock simu isitumike tena mmeshindwa wakat nimewapa imei no za simu na anaye tumia nimewapa kwan simu imesetiwa kila unapotoa line mwenye simu anapata ujumbe kama simu yake inatumika!hakuna technologia ya kuziunguza simu za wizi?

Hawawezi kukusaidia lolote. ila hiyo kitu inawrzekana kwa sababu kila simu ina imei yake . also mac address kwa smart phone.
 
Watanzania si waliambiwa wasusie network ya Voda kwa sababu ni kampuni inayomilikiwa na Mafiadi? How far have we gone?
 
Hiki kifurushi cha bila kikomo ndio balaaa kabisa. jaribu kujiunga ndio utajua nachomaaanisha.
 
Last edited by a moderator:
vodacom sasa nashangaa mmepotea kwenye intanet.mimi nipo morogoro mjini,intanet ipo slow sana huku.si tatizo langu tu.sasa sijaelewa kwanini.hili tatizo limeanza mwezi huu tu

Habari ndugu mteja, tafadhali tusaidie namba ya simu PM kwa mawasiliano zaidi ukitufahamisha eneo ulilopo na unapotumia unapata ujumbe gani.
 
Nimetumiwa text msg jana ndio nimeipata sasa hivi na taarifa zilizokusudiwa kunifikia ni irellevant saa hizi hili mnaliongeleaje? Na hata msg niliyojibu bado haijamfikia mlengwa mpaka tukapigiana simu.

Sihitaji tena huduma ya text msg ni upuuzi mtupu, wakati nilipokuwa mteja wa Tritel tulikuwa wateja tuna mkataba na Tritel ikitokea mtandao ndio umesababisha ukose biashara au upate hasara kulikuwa na kipengele cha kuwashtaki kudai fidia je nyinyi mna hicho kipengele?

Tafadhali tutumie PM taarifa hizi kwa msaada zaidi. Namba ya mtumaji, namba ya mpokeaji na muda ndugu mteja. Pole sana
 
Subiri nimeweka 1000 najiunga na chekabomba wanasema salio halitoshi ukicheki tena salio 897napont ukijiunga lands ya 800 haitoshi salio tena 756 napoint mpaka kero kasheshe wapigie watapokea kesho yake hawafai
Mkuu Good msoka, tafadhali hakikisha umezima Mobile Data kabla hujaongeza salio na fungua baada ya kununua kifurushi.
 
Last edited by a moderator:
Acheni kututumia SMS za nipashe zinakera sana
Kwanza hatukutaka kuunganishwa kwann mtuunge kwa nguvu.
Cku ya Leo tu had sa hv mshatuma SMS 16
Seriously mnaudhi.
 
Huduma ya internet (kwenye mobile phone) yenu slow sana, yaani data transfer ni very low per second.
Zamani ilikua nzuri sana, ila naona 'mmelewa' sifa ya kuwa kampuni kubwa ya simu za mkononi.
Rekebisheni hii, maana....
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Kuna maeneo hapa city center (Dar) network yenu ni shida sana.
Huwezi kuamini katikati ya jiji la Dar (maeneo ya St. Joseph Church mpaka TRA station) kupata mtandao wa voda ni changamoto..!!
Kama ha Dar hali ni hii, huko vijijini hali ikoje..??
 
Acheni kututumia SMS za nipashe zinakera sana
Kwanza hatukutaka kuunganishwa kwann mtuunge kwa nguvu.
Cku ya Leo tu had sa hv mshatuma SMS 16
Seriously mnaudhi.
Habari Ngokonii, tumewasiliana nawe kuhusu hili. Pole sana
 
Last edited by a moderator:
Huduma ya internet (kwenye mobile phone) yenu slow sana, yaani data transfer ni very low per second.
Zamani ilikua nzuri sana, ila naona 'mmelewa' sifa ya kuwa kampuni kubwa ya simu za mkononi.
Rekebisheni hii, maana....

Tafadhali tutumie namba ya simu PM na eneo ulilopo kwa mawasiliano.
 
Back
Top Bottom