Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania naomba nijue ni akina nani ambao namba zao zimefutwa na still hela ipo maana tuna ndugu ambao hatujui kama wana line ya voda je zile zinazobaki hua zinapelekwa wapi BAK

Habari Shark pesa huwekwa katika akaunti maalum, endapo una ndugu yako akaunti imefutwa mshauri afike dukani kwetu na pia kama ni mrithi pia anaweza kufika dukani kwetu na vithibitisho akiwa na namba ya mteja kwa msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Habari pole sana, tafadhali tutumie taarifa zako PM kwa msaada zaidi mkuu.
 
Voda wahuni hata nami hapa moro wameuza line yangu ya uwakala kwa wqtu wengine
Habari Gwaje, tunapenda kukufahamisha kuwa tatizo lipo kwa wakala mkuu uliyempatia taarifa zako. Tumekuwa tukishirikiana na mawakala katika hili kuhakikisha wanapatiwa Till zako. Tutumie taarifa zako PM kwa msaada tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Habari kyumana, hali hii hutokea pale ambapo simu inaendelea kutumia kutumia huduma za intaneti mara tu unapoweka salio. Tafadhali hakikisha umezima huduma za mtandao (Mobile Data) weka salio kisha nunua kifurushi na ufungue mobile data.
 
Last edited by a moderator:
Habari mkuu, itakuwa vyema tukapeana namba ya simu kwa msaada zaidi, tukifahamu siku/tarehe uliyonunua kifurushi itakuwa vyema.
 

Tafadhali jaribu tena sasa mkuu. Pole sana
 
Habari vodacom! Wiki iliyopita niliwasiliana nanyi kuhusu suala la mpawa, nikawapa na no yangu, mkasema mtanipigia simu, lakini hadi leo sijapata mawasiliano yoyote kutoka kwenu ili niweze kujua suala langu limefikia wapi, 0757 980 448. Naomba mnijibu ili niweze kujua km linawezekana au imeshindikana. Ahsante!
 
Mimi siwaelewi hawa voda! Kila nikinunua LUKU kwa njia ya m-pesa wanachelewa sana. Na ukiwauliza wanakuambia kuna tatizo kidogo upande LUKU TANESCO. Na wakati huohuo ukinunua kwa mtandao mwingine unapata muda huohuo. Na wao watakurushia token baada ya masaa 6 au siku inayofuata. Hebu hapa toeni jibu niwaelewe. Maana mkisema kuna tatizo kidogo upande wa TANESCO, hawa airtel ukinunu kwao wanakupa muda huohu. Wao wanatoa wapi?
 

Hii ni kweli kabisa. Wanakupa token baada ya ku complain mbona sijapata
 
Habari kyumana, hali hii hutokea pale ambapo simu inaendelea kutumia kutumia huduma za intaneti mara tu unapoweka salio. Tafadhali hakikisha umezima huduma za mtandao (Mobile Data) weka salio kisha nunua kifurushi na ufungue mobile data.

Nimeenda kujaribu ni kweli jibu lenu lipo sawa
 
Last edited by a moderator:
Nyie vodacom mbona mnaubaguzi kwa nin nasisi msituletee 3g huku boda kwetu wafanyakaz tupo wengi tunaitaji bhana pia sometimes network yenu inazengua msaada please
 

Nyie vodacom mbona mnaubaguzi kwa nin nasisi msituletee 3g huku boda kwetu wafanyakaz tupo wengi tunaitaji bhana pia sometimes network yenu inazengua msaada please mrongo border kaisho karagwe
 
Vodacom Tanzania
naomba kujua ni mtaji kiasi gani kinahitajika kupata lain ya M-PESA
 
Mi voda ndio kila kitu ila rekebisheni namna ya kuangalia salio la kifurushi yaani ni process ndefu utafikiri unatafuta dawa ya kienyeji kwa dk manyau nyau!
Bunini kwa kwa mfano mtu apige *149*04# aletewe salio lake fasta.
Vodacom Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Mimi lain yangu iko hewani ila mala nyingi watu wananilalamikia kila wakinipigia hawanipati limekua nitatizo lamuda mtefu hadi nafikilia kuacha kutumia mtandao wavodacom
 
habari, ningependa kujiondoa na huduma NIPASHE habari. Nimejaribu kujiondo kwa njia ya kutuma sms

"ONDOA au STOP" kwenda 15501. Inakuwa failed naomba msaada
 
habari, ningependa kujiondoa na huduma NIPASHE habari. Nimejaribu kujiondo kwa njia ya kutuma sms

"ONDOA au STOP" kwenda 15501. Inakuwa failed naomba msaada

Mimi SIM card yao nimeacha kuitumia sababu ya hizo sms za NIPASHE HABARI ambazo wanakata hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…