Kwanza habari za kazi kwenu nyote mnao husika?
Pili niende kwa linalo nisibu haijalishi mtanisaidia ama mtapotezea,mhimu kwangu mlitambue. Mnapo anzisha huduma zenye kulenga kumsaidia mteja kweli mlenge ktk hilo,siyo mnaanzisha ktk mfumo huo kumbe mpo ktk mfumo wa ninyi kujiingizia kipato{mauzo} kwa kiwango cha juu. Hapa naomba nigusie mfumo wenu wa cheka na hasa hii cheka bombastick na hasa inayo husu mitandao yote. Nimekuwa mhanga wa hili kwa kipindi kirefu sana. Imani kwamba dk.zote ninazo nunua ninazitumia haipo tena hapa kuna usanii flani unafanyika na mbaya zaidi ni kama umenunua kifurushi cha wiki au mwezi hapo sahau kufika nacho mwisho.Na kwa kuthibitisha hilo nimejaribu kununua kifurushi cha aina hiyo kwa mtandao mwingine na kingine chenye thamani kubwa tena kimoja kwa ajili ya off net & on net na kingine kwa ajili ya on net tu kwa upande wenu bado hivi vya kwenu vimeisha haraka ilihali kile cha mtandao pinzani mpaka leo natumia. Hebu jitathiminini kwa hili.
Lakini pia mna ugonjwa wa mtu kupiga simu kama ana kifurushi na kika isha ndani ya maongezi kama ana salio mstoe taarifa na wakati mwingine hata akipiga simu nyingine na pale salio liishapo tu ndiyo mnatuma taarifa ya kuisha kwa kifurushi. Maana yake nikanunue vocha nyingine. Kama hiyo ndiyo ilikuwa budget yangu ya vocha kwa siku,wiki ama mwezi! Niende nje ya budget si ndiyo? Na kama niko sehemu ambayo upatikanaji wa vocha ni mgumu? Nikae bila mawasiliano ama niwe nasubiri kupigiwa? Au ndiyo kunipeleka ktk huduma ya kunilazimisha nikope kutoka kwenu ili mtengeneze faida mara mbili kwa kupitia vocha nitakayo inunua kulipa na kunikata zaidi kutokana na mkopo wenu?
Hebu tuchukulieni kama wateja wenye kustahil huduma bora na siyo manyanyaso kwamba wamesha ingia wataenda wapi?
Ni hayo tu mnaweza kufanyia kazi ama kupotezea kama ikionekana hayana mashiko kwenu!