Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Sio uongo jamani VODACOM....sasa wamekuwa keroooooo kabisa,huduma ya internet ni kimeo kupitiliza.Kama mpo humu ndani hebu jaribuni kulishughulikia hili.Mimi nimesha limesema hili hata kuwapigia customer care,na kupost comment kwenye uzi wao flani humu ndani lakini ni chenga...mara tutajie eneo ulilopo mara tunakutumia configuration right now...ACHENI UBABAISHAJI VODACOM.
Mlianza vizuri sana ila sasa mnapoteza dira kabisa....AU NDO ILIKUWA NGUVU YA SODA,KUVUTA WATEJA WENGI...KISHA KUONYESHA MAKUCHA YENU:angry:.
 

Mkuu kuna watetezi wao humu, wateja wakilalamika na kutoa madukuduku yao utashangaa kuona malalamiko ghafla yamefutwa. Hata sasa usishangae haya malalamiko yako kufutwa au nilichochangia juu ya hoja yako kufutwa.
Kwa ujumla voda wamekua matapeli sana siku hizi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Tunawashauri wajirekebishe. Si uungwana kuwa-pm mamoderator wa hapa jf ili waondoe malalamiko ya wateja. Ukweli lazima usemwe.
 
mi asa hv natumia sana airtel toka wapunguze vifurushi vy a internet siwapendi kabisa
nlikua sipendi kutumia line mbili ila imenibidi
 
mi asa hv natumia sana airtel toka wapunguze vifurushi vy a internet siwapendi kabisa
nlikua sipendi kutumia line mbili ila imenibidi

Airtel ndo mpango mzima, hayo mavodacom ni taabu tupu.
 
Habari Mkuruka pole sana, tutapenda kupata namba yako ya simu ili kuweza kuangalia hili katika mifumo yetu.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu tweenty4seven angalia salio kwa kupiga *147#. Hii hutokea endapo unakuwa na kifurushi zaidi kimoja.
 
Last edited by a moderator:
Habari Mkuruka pole sana, tutapenda kupata namba yako ya simu ili kuweza kuangalia hili katika mifumo yetu.

Wewe umeambiwa ni tatizo la wateja wengi unakomalia upewe namba ya mteja mmoja kweli mnashindwa kurekebisha system zenu in general? Mtabaki na wasiong'amua kama ndo mnakwenda kwa mtindo huo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tweenty4seven angalia salio kwa kupiga *147#. Hii hutokea endapo unakuwa na kifurushi zaidi kimoja.

Niliweka 15,000 alhamisi iliyopita mkanipa dk 230 na mb 600 kufika jmosi mchana simu imeishiwa salio.nina hakika sijatumia dk100 za maongezi sasa hapo kama si uwizi ni nini
 
Last edited by a moderator:
Anko Kidevu;10790125]voda kunaeneo lipo moshi.KDC hakuna network mtu ukimpigia haumsikii na nenden mkaulize wakazi wa hapo watawaambia kero zao inakera sana
Habari Anko Kidevu, unaweza kutusaidia namba ya simu ya mkazi yeyote wa eneo hilo kwa msaada zaidi.
 


Habari Gibeath-Elohimu namna pekee ya kutatua matatizo ya wateja ni kuwa karibu nao na hili ndilo lililotusukuma kuwa na akaunti JamiiForums, tungependa kuichukua changamoto na kuifanyia kazi hivyo tunaomba ututumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli ma Agent Wa M pesa wanakera sana Nimeomc uwakala toka mwaka jana mwezi wa 11 hadi leo sijawai kupata na cha kushangaza kumb wameuza line yangu kwa mtu mwingine na nimekuja kulibaini hilo swala mwaka huu mwezi wa tisa. Jaman Vodacom kwanin mnajiwekea sifa mbaya?? Hivi hawa mawakala mnatumia criteria gan kuwapata?? Namba mnisaidie kuswap line yangu mapema.
 

Kwanza niseme uharaka huu ambao mmeutumia kuja kujibu na kutatua hii changamoto ndio unaotakiwa.Pili kiukweli nasita kutoa number yangu tena maana hii haitakuwa mara yangu ya kwanza kutoa number yangu kwenu(mwisho nikaoneka msumbufu,ili hali ni haki yangu).Kama mko makini pitieni uzi wenu kule nimetoa number tena kwa jina hili hili.Tatizo liko wazi yakuwa siku hizi INTERNET yenu iko chini sana hasa kwa wanao tumia simu(yaani mpaka utegee nyakati za usiku) tofauti na hapo nyuma. Mimi niko KIMARA kama shida ni minara ya eneo husika au mtandao kuwa chini kwa eneo husika ni WAKATI SASA WA NYINYI KULISHUGHULIKIA HILI.

Natanguliza shukran!
 
Pole sana fngowi tafadhali tutumie taarifa zako za uwakala PM kwa msaada zaidi na jina la wakala mkuu uliyepeleka maombi kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…