Mkuu skype, hao airtel ndo wezi kupindukia. Hawakunasa tuu. Nilinunua bundle nikapata mb127, ndani ya dakika 28 za kusoma email hizo mb zimeisha na wakatafuna airtime yangu laki na sitini na tano! Kupiga customer care hamna kitu. Kwenda ofsn kwao wakasema watarudisha network yao ilikuwa na shida. Baada ya siku2 hawajarudisha, nikaandika email wakajibu nilitumia zote mwenyewe. Nikawaambia wanitumie details nilivyotumia hela zote hizo kwa kusoma email tena hata nusu saa haijafika wakadai tcra wanakataza. Nasubiri salio langu liishe nitupe na line kabisa!