Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Kwa nini huduma ya 3G inakuwa haipatikani kati ya saa 1 jioni hadi saa 3 usiku maeneo ya Ilemela Mwanza?
 
Voda huduma Zime dolora a mtu anatuma SMS inakaa zaidi ya masaa 3 had 4 au anakupigia sipatkani imekuwa kero. Kama kuna uwezekano ongezen booster za mtandao ili kupunguza msongamano (network jam)
 
Jamani nyie vodacom mmenikera na mnaendelea kunikera kwa kunikata hela za hivyo vichwa vya habari vya nipashe nimewapigia zaidi ya mara sita mnaahidi kutoa ila hamtoi nmeweka vocha sijaitumia ila sahivi imebaki nusu afu hao customer care wenu kila anayepokea Ananipa maelekezo yake mnanichefu kesho nikiamka salama hilo vumbi nitalowawashia mtajuta
 
Jamani vodacom mimi kama mteja wenu naomba mtuwekee kifurushi kipya cha mb na sms tu kwa sisi tunaoshinda mtandaoni. Hatuna mda wa kupiga cm. Mtujali tafadhari.
 
Kilio changu mimi ni swap zinachelewa mawakala wetu wanasubiri sana na muda wote wanaposubiri muda wote hawafanyi kazi cha kusikitisha zaidi kumekuwa na mlolongo mrefu tumeni watu wakachungumze
 
Wajanja night irudi 4gb itakua poa sana halafu gharama za.vifurushi kwenda mitandao yote mmepungza dk na bando sio poa wala nini bora mngeacha vilevile au mngeshusha mitandao mingine isingewakamata daima..
 
Kwakweli mtandao mkubwa kama Vodacom inasikitisha na kuaibisha pale inapoweka swala usanii ndani ufanisi wao wa kazi, nikianza na dk za cheka kuna usanii mtupu unaoendelea hapo ndani mpaka uwizi wa dk, mbili mkijua mnahitaji wateja wengi boresheni huduma zenu yaani network kwani hapo kuna kero kubwa sana ktk hilo, internet yenu ni tatizo kubwa ipo slow sana sana, namalizia na wafanyazi ndani ya kampuni sio wote ila wengi wao wanafanya kazi kama wana hisa ndani, wanafanya kwa ulegevu na kuangalia watu kama nyanya mbichi alimradi kakaa ktk kiti cha huduma jirekebisheni. Vodacom bado kazi ipo
 
Mkuu skype, hao airtel ndo wezi kupindukia. Hawakunasa tuu. Nilinunua bundle nikapata mb127, ndani ya dakika 28 za kusoma email hizo mb zimeisha na wakatafuna airtime yangu laki na sitini na tano! Kupiga customer care hamna kitu. Kwenda ofsn kwao wakasema watarudisha network yao ilikuwa na shida. Baada ya siku2 hawajarudisha, nikaandika email wakajibu nilitumia zote mwenyewe. Nikawaambia wanitumie details nilivyotumia hela zote hizo kwa kusoma email tena hata nusu saa haijafika wakadai tcra wanakataza. Nasubiri salio langu liishe nitupe na line kabisa!
 
Vodacom=CCM Msipoteze mda wenu kulalamika Unadhani CCM pesa itatoka wapi kwanza Vodacom wanakiburi utadhani nienzi ya ttcl leo iko wapi na hawa watakuja potomoka tu
 
Mkuu skype, hao airtel ndo wezi kupindukia. Hawakunasa tuu. Nilinunua bundle nikapata mb127, ndani ya dakika 28 za kusoma email hizo mb zimeisha na wakatafuna airtime yangu laki na sitini na tano! Kupiga customer care hamna kitu. Kwenda ofsn kwao wakasema watarudisha network yao ilikuwa na shida. Baada ya siku2 hawajarudisha, nikaandika email wakajibu nilitumia zote mwenyewe. Nikawaambia wanitumie details nilivyotumia hela zote hizo kwa kusoma email tena hata nusu saa haijafika wakadai tcra wanakataza. Nasubiri salio langu liishe nitupe na line kabisa!

Mkuu, kwanza pole na masahibu yaliyokukumba. Inaonekana sasa mitandao karibu mingi ya simu ni wezi hasa wakiongozwa na voda huku wengine wakifutia.
 
Vodacom wamezidi,juzi nimenunua airtime 20000 jioni ya saa mbili asubuhi zote hamna,customer care simu haijibiwi napigiwa muziki tu
 
Ninahitaji laini ya Uwakala wa M.pesa nifanyeje niweze kupata na inaweza kuchukua muda gani kupata hiyo laini. nipo Muleba Kagera.
 
Kumekuwa na usumbufu mwingi sana usiokuwa na lazima hasa kuhusu M-Pesa kuwezeshwa baada ya ku-renew line, unaporipoti tatizo lolote kama suala la network, modem na mambo mengine. Wao wanamaneno yao ya kukuridhisha kama vile tumeripiti idara husika, tumenashughulikia baada ya masaa 24 au 48. Huu usumbufu unachosha. Mnafanya biashara badilikeni hamko pekee yenu wapo washindani wenu pia. Any way njia rahisi ni kuwahama tu kama hamtajirekebisha

Vodacom Tanzania
 
Last edited by a moderator:

Back
Top Bottom