Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom wamezidi,juzi nimenunua airtime 20000 jioni ya saa mbili asubuhi zote hamna,customer care simu haijibiwi napigiwa muziki tu
Pole sana, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Ninahitaji laini ya Uwakala wa M.pesa nifanyeje niweze kupata na inaweza kuchukua muda gani kupata hiyo laini. nipo Muleba Kagera.
Habari,ili kuwa wakala wa M-PESA unatakiwa kuwa na leseni ya biashara, TIN namba na kitambulisho kisha unafika Vodashop kwa msaada zaidi.Mtaji ni Tsh 500,000/= na zoezi linakamilika ndani ya wiki 5
 
Make your network troubleshooting .since last year I had made my troubleshoot and come up with the solution by changing my phone model up to now with smartphone still same same problems.
 
Ninyi yaani mnakera sana na internet yenu ilivyo slow.
 
Kwa kweli kazi imewashinda..jana ile kifulushi nimeweka cha elfu 20 cha mwezi bila kikomo,sijadownload chochote lakini leo imeingia msg inasema nimemaliza kifulushi na nitapata huduma kwa kasi ndogo,kuangalia salio la kifulushi sina MB hata...nimepiga simu mtu mmoja mtoa huduma anasema anawasiliana na makao makuu sehemu husika ya kua yeye hana cha kunisaidia na kudai kua watu wa makao makuu watanipigia kitu ambacho sijapokea call yao mpaka sasa,kwa kweli magadhabika sana na huu mtandao,isingekua huduma ya M Pesa kutuma vijisenti huko vijijini kwetu leo hii line yenu ningeikata na familia yangu yote ningeilazimisha ibadili mtandao
 
Tunaomba radhi kwa usumbufu ulioupata. Akaunti ya M-Pesa hufungwa kwa muda lengo ni kuweka usalama wa Pesa za mteja na atatakiwa kuthibitisha taarifa zake.
 
voda mtandao wenu these days unAsumbua sana internet yaani mi hadi nAona kero
 
Pole sana ndugu mteja, tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa msaada zaidi na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Make your network troubleshooting .since last year I had made my troubleshoot and come up with the solution by changing my phone model up to now with smartphone still same same problems.
Morning Edson, kindly let us know the problem that you are facing. Thanks
 
Huu ni utapeli hivi ni nini maana ya unlimited maana si wengine wageni
Habari ngivingivi, ni kwamba kifurushi kinakuwezesha kutumia huduma za intaneti kwa muda wote uliolipia, kwa maana kwamba ukinunua cha siku 30 na ukatumia kwa siku 8 kifurushi kikaisha utaweza kuunganishwa kwenye mtandao kwa siku 22 zilizobaki hadi muda wa mwisho uliolipia. Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Hivi unakuwa karibu kabisa na minara ya Vodacom na bado mawasiliano ni ya shida, network strength iko chini kabisa kiasi kwamba matumizi ya simu kawaida ni shida, internet ndo hakuna cha 3G wala nini, Moderm hazina kazi! tunaomba turekebishiwe hili tatizo. Ni wilaya ya chunya - Mbeya eneo la kiwanja.
 
Mnatuibia sana like hizi simu mpya smart kiki mlisema ---- memory card GB 4,SMS za bure na mb lakini matokeo yake wizi mtupu me nimenunua akuna lolote
 

Yaani kiukweli voda kwa sasa huduma zao wanazitoa kwa kubahatisha, hata mafreelancer wao wanawaibia kweli... ukienda kuuliza majibu unayopewa hata hayaeleweki wala hayaridhishi... Ushauri utawala wa voda kuweni macho kutatua kero za mafreelancer na wateja wenu kwa muda muafaka.. kumbukeni hao hao wanao nyanyasika ndiyo wanawaingizia nyie kipato......
 
Pole sana, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.
 
Kuna tatizo la voice call morogoro unapopiga kwenda nje ya morogoro mjini simu zinakata kata toka jana.

Angalieni tatizo liko wapi, currently natumia mtandao mwingine ili kuokoa kazi zangu ila mtakaposhughulikia basi tutarejea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…