Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mimi naomba kuuliza juu ya vifurushi vya Blackberry kupitia Vodacom. Nina watu watatu nimewanunulia simu za Blackberry wanahangaika kujuwa kama kuna kifurushi cha vodacom kupitia blackbery kitakacho wawezesha kupata Internet na kupiga pamoja na sms baadala ya kununua cha internet tupu. Nilishawahi tumia vodacom Complete ambayo ilikuwa ni internet tupu na nisingewashauri wachukuwe hicho as wanahitaki kupiga simu pia.

Natanguliza shukrani.
 
Mimi naomba kuuliza juu ya vifurushi vya Blackberry kupitia Vodacom. Nina watu watatu nimewanunulia simu za Blackberry wanahangaika kujuwa kama kuna kifurushi cha vodacom kupitia blackbery kitakacho wawezesha kupata Internet na kupiga pamoja na sms baadala ya kununua cha internet tupu. Nilishawahi tumia vodacom Complete ambayo ilikuwa ni internet tupu na nisingewashauri wachukuwe hicho as wanahitaki kupiga simu pia.

Natanguliza shukrani.
 
nisaidieni jamani voda. jana nimerudi niko tungi sikumbuki niliiweka wapi naomba msaada wenu mnipigie tafadhali kama ninaweza kuiswap kwa wakala yyte wa mpesa. niko dar yombo kwa alimboa
 

mbona ize tu! star 149 star 01 then unachagua internert & bb10. kwa wasiojua blackberry si kama smartphone lazima uwe subscribed uweze kutumia net. nadhani nimeeleweka kaka. kwa msaada zaidi 0757430913
 
Nashukuru Sana Mkuu!!!!!!!!!!! Nimewafikishia maelezo na wameyafuata na kufanikiwa maana mimi sipo huko bongo.

Ubarikiwe!!!!!!!!!
 
mbona ize tu! star 149 star 01 then unachagua internert & bb10. kwa wasiojua blackberry si kama smartphone lazima uwe subscribed uweze kutumia net. nadhani nimeeleweka kaka. kwa msaada zaidi 0757430913


Nashukuru Sana Mkuu!!!!!!!!!!! Nimewafikishia maelezo na wameyafuata na kufanikiwa maana mimi sipo huko bongo.

Ubarikiwe!!!!!!!!!
 
kwanini kuunga kifurushi cha mitandao yote kinasumbua sana hata kams salio lipo utaambiwa halipo hivi kweli mmejipanga kweli .
Habari Bedo, hii inatokea pindi unapokuwa umefungua huduma za Intaneti kisha ukaweka salio, unachotakiwa kufanya ni kuzima huduma za Intaneti ongeza salio na nunua kifurushi kisha fungua huduma. Ahsante
 
mbona hapa ihanda -mbozi hatupati internet ya uhakika pia tigo wana 3g network lakin vodacomo ni edge tu hebu tusaidieni hili wateja wenu tigo wanawapiga bao.
Tafadhali tutumie taarifa zaidi PM, ukitupatia namba ya simu na namba mbadala.
 

Ahsante kwa kutuandikia Bayyo na kutupatia mrejesho wa huduma zetu. Tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Kuna tatizo kubwa la mtandao huku chuo kikuu cha dodoma hasa college ya humanities unaweza k utuma sms asubuhi mtu akaipata kesho yake je tatizo ni nini? Tunawaomba mfike na kulitatua kwani imekua ni kero kubwa sana
Habari, tafadhali tunaomba ututumie sample numbers zenye tatizo hili, itakuwa vyema ukitupatia namba ya mtumaji na namba ya mpokeaji na muda ambao ujumbe ulitumwa. Poleni sana
 
Ile bundle ya 5gb kwa mwezi ilikua very fast and efficient. This new unlimited thing is just not working.
Hi Sceptic123, the new unlimited bundle gives you a true freedom to surf till the end of validity. Please clarify how is it not working?
 

Habari marimba, suala hili bado linashughulikiwa na tunaimani huduma itakuwa sawa siku chache zijazo. Pole sana
 
Mimi sijapenda njia yenu mpya ya ku renew line inapopotea. eti mpaka uwe na kumbukumbu ya tarehe ya mara ya mwisho ulipoweka voucher?? Isitoshe mnadai mteja akumbuke transactions zake zote za m pesa kitu ambacho ni kigumu sana kwa watu wengi. Pia gharama za ku renew line ni kubwa sana. Unaambiwa na wakala kununua line ni 2,000 na ku renew ni 5,000 hivyo kufanya jumla kuwa elfu 7. Mpaka leo sina line ya voda kisa nimeshindwa ku renew. Naombeni msaada wenu voda bado naitaka jamani.
 
bundle zenu wizi mtupu,unannua kifurushi cha internet cha wiki,kila hutumii net unazima data na usiku wakati wa kulala unazima lakini baada ya Sikh tatu au NNE unaambiwa kifurushi kimeisha...ovyo kabisa!
 
Nimefanya kazi kwenye kampuni mbali mbali
za simu hapa nchini kwa muda wa zaidi ya
miaka 10, kabla ya kuamua kujiajiri
mwenyewe. Katika muda wote huo
nimeshuhudia kampuni hizi zikiwaibia wateja
kwa namna mbalimbali. Nimekaa na huu
ushahidi kwa muda sasa lakini naona roho
inanisukuma niuanike hadharani mbele za
watanzania ili wafunguke macho na kufahamu
UFISADI huu unaofanywa na kampuni za simu
hapa nchini. Nitaanika wizi wote kadri
nitakavyoweza kuukumbuka hapa:
Huduma za bure
Kuna hizi huduma ambazo wanaziita huduma
za “BURE” kana kwamba zinapatikana bure
wakati si kweli! Kwa mfano, wateja hutumiwa
SMS zinazowadanganya kwamba wanaweza
kupata huduma za bure na ili wazipate
wanaelekezwa kutuma ujumbe kwenda kwenye
namba fulani. Na mteja akisharogwa akatuma
ujumbe kwenda kwenye namba husika, imekula
kwake! Nyingi ya huduma hizi zinzoitwa za
bure hugharimu fedha na mara ujiungapo
hujikuta unakatwa salio lako kimya kimya. Ni
mara nyingi mtakuwa mmewahi kusikia mtu
akilalamika kwamba salio lake
limepungua….unaweka airtime ya Tsh 1000 leo
bila kuitumia, ikifika kesho unakuta zimebaki
sh 350! Tsh 650 zimeenda wapi? Zimekatwa
kwenye zile huduma za “BURE” ulizotangaziwa.
Promosheni feki
Promosheni nyingi zinazoanzishwa na
makampuni ya simu zinalenga kuwanyonya na
kuwakandamzia wateja. Mfano halisi ni pale
wateja wanapotangaziwa kwamba huduma ya
FESIBUKU inapatika bure! Thubutuuu! Hakuna
kitu cha bure nchi hii, ndugu yangu. Huu ni
wizi wa mchana! Kupona kwako ni pale
utakapotumia hiyo huduma ukiwa hauna salio
kwa kuwa huwezi kupata access ya huduma
husika (kama vile fesibuku, twita, nk). Ikiwa
utafungua huduma hiyo ukiwa na salio, salio
lako lote litakombwa sawia! Kuna mtandao
mmoja wa simu unajinadi kwamba unatoa
huduma ya fesibuku bure wakati ni uongo
mtupu. Ingia kwenye hiyo fesibuku uone
utakavyoliwa fedha! Aidha kuna mtandao
mmoja uliwahi kuwa na fesibuku ya bure siku
za nyuma (kama mtakumbuka). Kwa muda
fulani huduma hii ilikuwa ikipatikana bure
kabisa. Kumbe ilikuwa ni janja ya
nyani…..baadaye ile “bure” ilifutwa kimya
kimya, wateja wakaendelea kukamuliwa kama
kawaida na mpaka leo hawajawahi
kuwataarifu wateja wao kwamba hiyo “bure”
imesitishwa! Kuna wateja wengi sana, hasa wa
kule vijijini, ambao wanaendelea kukamuliwa
kwa kujidanganya kwamba huduma ni ya bure
hadi leo, kumbe ilishasitishwa kitambo sana!
Ulaghai wa Kimangungo
Kuna wakati ambapo makampuni ya simu
hupandisha tariffs kimya kimya bila
kuwataarifu wateja wake na kuendelea
kuwaibia bila kujua. Mwaka 2006 gharama za
kupiga simu, kutuma sms na kutumia data
zilipandishwa kinyemela na wateja
wakaendelea kukamuliwa fedha kimya kimya
hadi pale baadhi yao waliposhtukia dili na
kuja juu. Aidha, prosheni fulani
zinapoanzishwa, kama vile punguzo la
gharama za kupiga simu nyakati za usiku,
pindi zinafikia tamati wateja hawapewi
taarifa na kujikuta wakitumia fedha zaidi ya
matarajio yao. Promosheni inapoisha kampuni
hizi huwakataza wafanyakazi wake
wasiwaambie wateja ili waendelee kukamuliwa
fedha kilaghai. Huu ni wizi, tena wa mchana
na hauna tofauti na ufisadi wowote ule.
Kutotoa taarifa kwa wateja kwa makusudi
Wateja wanapojiunga kwenye vifurushi
mbalimabli huletewa taarifa immediately via
SMS kwamba wamefanikiwa kujiunga lakini
kifurushi kikiisha ama wateja huchelewa
kutumiwa meseji ya taarifa au hawatumiwi
kabisa. Hili tatizo huwakumba zaidi wale
wateja wanaopenda kubaki na salio kubwa
kwenye simu zao. Kwa mfano, mtu unanunua
vocha ya Tsh 2000 kisha unanunua kifurushi
cha Tsh 500 na kubakiwa na Tsh 1500 kwenye
simu. Pindi kifurushi cha 500 kikiisha
hutatumiwa ujumbe wowote hadi utapokuwa
umekausha 1500 zilizosalia kwenye simu. Huu
pia ni wizi wa mchana na unaofanywa kwa
makusudi na kampuni za simu hapa nchini.
Ninao ushahidi usiokuwa na mashaka katika
huu wizi wa makusudi.
Njia nyingine inayotumika kuiba hapa ni
kutotoa call details pindi upigapo simu.
Ukimaliza kupiga simu ukiangalia call details
unakuta inasoma 00:00:00! Details hizi
zinafichwa kwa makusudi ili kujenga
mazingira ya wizi. Kwa mfano mtu unaongea
kwa dakika 3, wao wanakata dakika 4.30 na
kukuibia dakika 1.30! Matokeo yake unakuta
muda wa hewani uliopewa wakati wa kujiunga
umeibiwa na kampuni kwa maslahi yake
binafsi. Lakini pia kuna wizi mwingine huu
hapa: – unaponunua kifurushi hupewa dakika
ambazo ungetegemea zizotozwe kwa sekunde
(per second billing) lakini badala yake
hutozwa kwa dakika (per minute billing)
kinyume cha mkataba kwa lengo la kumkamua
mteja kiujanja. Huu ni wizi na haukubaliki
hata kidogo.
Kuvuruga mawasiliano kwa makusudi
Kuna wakati wahandisi wa kampuni husika
hupewa jukumu la kuvuruga mawasiliano ya
wateja ili watumie muda mwingi na pesa nyingi
kwenye maongezi. Inakuwaje hapa? Inakuwa
hivi: Ukimpigia mtu yeye anakuwa anakusikia
lakini wewe humsikii au vice versa. Hii
husababisha kutumia muda mwingi kuelewana
wakati huo salio likinyonywa kama kawaida –
hata kama mkichukua muda mwingi kuelewana
salio hutafunwa sawia! Njia nyingine
inayotumika hapa ni kuvuruga access to
customer care ili unapokuwa umepatwa na
tatizo usiweze kuwafikia watu wa huduma kwa
wateja kupata msaada. Hii ndio sababu 90%
ya wateja wenye matatizo genuine hawaipati
namba 100. Mtu unaweza kupiga siku nzima na
usiunganishwe kuongea na mshauri. Hatimaye
wengi wao hukata tamaa na kuamua kukubali
“kuliwa”!
Hii ni sehemu ya ushahidi ambao
nimeukusanya while working with different
mobile companies in Tanzania. Siwezi kuwa
adui kwa kusema ukweli.
Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…