Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ni kwanini mnafadhiri blogs ambazo hazina maadili, zimejaa matusi na mambo mengi yasiyo mazuri kwa jamii yetu mfano u-turn blog inayomilikiwa na mange kimambi? Mnatudharirisha sisi wateja wenu, fedha zetu tunazowachangia mnaenda kufadhiri matusi huko ni kukoseana adabu. jaribu kuangalia upya sera zenu na vigezo vyenu mnapokuwa mnafadhiri hizo blogs.
 

Nasoma blog nyingi lakini nadhani yuke dada akili yake si nzuri ni aibu kwa kampuni kama Voda kudhamini upuuzi ule, lakini wanajua wenyewe vigezo wanavyotumia lakini ni aibu.
 
Nasoma blog nyingi lakini nadhani yuke dada akili yake si nzuri ni aibu kwa kampuni kama Voda kudhamini upuuzi ule, lakini wanajua wenyewe vigezo wanavyotumia lakini ni aibu.

Alipata sponsorship ya Vodacm kupitia uswahiba wake na Mwamvita Makamba.

Nchi hii haijarishi unajuwa nini bali unamjuwa nani?

Line ya Vodacom nimeshaitupa chooni mpaka wajirekebishe ndio nitafikiria kurudi.
 
Alipata sponsorship ya Vodacm kupitia uswahiba wake na Mwamvita Makamba.

Nchi hii haijarishi unajuwa nini bali unamjuwa nani?

Line ya Vodacom nimeshaitupa chooni mpaka wajirekebishe ndio nitafikiria kurudi.

Wanapaswa wapitie kwa umakini blogs wanazo zisponsor, hata kama alipata sababu ya urafiki lakini hapana anamwaibisha rafiki yake+ voda. Mtu mwenye akili thmamu huwezi kuwa na rafiki kama yule.
Kwakweli mi Voda inanisaidia hasa upande wa Sim Banking kwa shughuli zangu imenipunguzia karaha za kwenda Crdb mara kwa mara kwa hilo nawapongeza.
 
Aisee Vodacom Tanzania kuna tatzo mfano mimi nilituma pesa yangu kutoka accounti yangu m.pesa kwenda bank ya posta siku ya jumamos saa moja na dk14 jion m.pesa wakadhibitisha kua pesa imeenda bank maajabu mpaka sasa pesa haijafika bank napiga custurmer care kila mmoja na jibu lake kiukweli vodacom mmenikera mno.
 
Jamani mtandao wenu siuelewi ata kidogo, nikijiunga kwenye kifurushi then nikiitaji kuconnet kwenye internet inaonekana ipo lakini haiconnect ata kidogo na kifurushi kinakwisha sijui ni kwanini.
 
Vodacom Tanzania..

Hivi wateja wenu wa Internet tumewakosea nini????

Naona mmeamua kupunguza MB kwenye vifurushi vyenu...

Mf. Kifurushi chs T.shs. 899/=..

Baada ya kupunguza
.......................................
Hongera!Umenunua dakika 18 za kupiga mitandao yote,SMS 500 mitandao yote TZ na 10MB zitumike hadi 2014-11-18.Piga *147# kujua salio.

Kabla ya kupunguza

Hongera!Umenunua dakika 18 za kupiga mitandao yote,SMS 500 mitandao yote TZ na 100MB zitumike hadi 2014-11-14.Piga *147# kujua salio.

NB;
Mmepunguza kwa 90%....
 
Nime note shida hii kwa takriban week 2 mfululizo kwa mwezi huu wa Nov. Simu za Airtel na Tigo naambiwa mtumiaji hapatikani. Nikipiga kwa Airtel nampata
Tunaomba sample numbers tafadhali na namba yako ya simu kwa msaada zaidi.
 
Habari Samwel, tafadhali tutumie namba yako ya simu PM na muamala husika kwa msaada zaidi. Pole
 
Vodacom mi mpaka nime wahama .....yaani naweka vocha sipigi simu wala situmi sms
Wala siperuz nokia 1200tochi
Ila pesa inapungua 100tzs kila baada ya masaa matatu
Kama mimi muongo yeyote aliyeko arusha achunguze.....
.....kingine kifurushi cha kuongea kinajihesabu speeed ya ajabu.....yaani
Nlijiunga
Tigo dakika 20 na voda dakika 20
Nikachukua simu zote mbili nikazipiga kuzifanyia majaribio...
Yaani tigo ipo dakika ya 16:37
Voda ilishamaliza dakika zote
Acheni wizi.....
......kingine internet yenu kwa sasa ni mbovu tz nzima....tuboresheeni ongezeni minara mijini.....
Kwa sasa ni hayo tuu ila yapo mengi mno
 
Habari Samwel, tafadhali tutumie namba yako ya simu PM na muamala husika kwa msaada zaidi. Pole

Mbona maswali mengine mnayaruka hamjibu? Wababaishaji wakubwa nyinyi hamtopata hata mia kutoka kwangu endeleeni kudhamini machangudoa.

Mlivyoacha kudhamini miss Tanzania niliwaona mna akili sasa hivi upunguwani umewarudia.
 
Jamani mtandao wenu siuelewi ata kidogo, nikijiunga kwenye kifurushi then nikiitaji kuconnet kwenye internet inaonekana ipo lakini haiconnect ata kidogo na kifurushi kinakwisha sijui ni kwanini.

Pole sana, unatumia simu aina gani tafadhali. Angalia kama simu yako ina mpangilio sahihi wa Intaneti.
 
Hawa siku hizi ni wajinga kinoma ... bundle zao za kijinga.. wanatoa bundle nzuri wanaanza kuharibu pole pole... mm nawahama hawa wajinga
 

Hawa hovyo sana... wanazani hatuna line zingine tena wengine wana bundle nzuri tu... mm MB 50 znanisaidia nn... wakati mitandao mingine naweza nkapata MB 120 kwa hiyo hela kwann nihangaike kununua vocha ya voda... voda wanakera sana...
 
Vodacom mmepunguza sana vifurushi vya Internet. Kama mnajali wateja wenu mliangalie hilo. Yaani imekuwa gharama kubwa sana kuwa na kifurushi cha kutosheleza matumizi binafsi ya Internet kwa wiki kwa mwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…