Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hawa hovyo sana... wanazani hatuna line zingine tena wengine wana bundle nzuri tu... mm MB 50 znanisaidia nn... wakati mitandao mingine naweza nkapata MB 120 kwa hiyo hela kwann nihangaike kununua vocha ya voda... voda wanakera sana...


Hawa jamaa walianza kwa kupunguza dk... Mf. t.sh 14,000 ilikuwa unapata dk 600 za kupiga mitandao yote kwa siku 30.. Wameshusha hadi dk 230....

Huu ni uhuni wa wazi wazi.
 
Ziro kabisa vodacom pesa yangu mmetapeli yaani aisee natuma pesa bank mnajisevia mfukoni??watanzania wenzangu tuogopeni hii mitandao km ukoma tena kwenye kutuma pesa au kutoa pesa kupitia m.pesa ni patapotea!!
 
voda mnazingua sanaaa,,,, kwann mnakata kias flan cha hela pale m2 anapofanya miamala ya NMB mobile wakat mitandao mingine n bure??? Mr vodacom nakutorokaaaaaaaaaaaaa
 
Habari Dragondreamx, tafadhali tusaidie namba ya simu tuweze kufuatilia suala hili na tupeane msaada kuhusu tatizo la Intaneti.
 
Vodacom mmepunguza sana vifurushi vya Internet. Kama mnajali wateja wenu mliangalie hilo. Yaani imekuwa gharama kubwa sana kuwa na kifurushi cha kutosheleza matumizi binafsi ya Internet kwa wiki kwa mwezi.

Habari ndugu mteja, kwa sasa vifurushi vya Intaneti vimepunguzwa gharama kuliko ambavyo ilikuwa kabla, Kwa Tsh 6000 unapata kifurushi cha siku 7 bila mpaka wa matumizi. Kwa wenye matumizi makubwa kuna kifurushi cha Tsh 30,000 kwa 20GB na cha elfu 20,000 bila mpaka mwezi mzima.
 
Ziro kabisa vodacom pesa yangu mmetapeli yaani aisee natuma pesa bank mnajisevia mfukoni??watanzania wenzangu tuogopeni hii mitandao km ukoma tena kwenye kutuma pesa au kutoa pesa kupitia m.pesa ni patapotea!!

Habari Samwel, pesa yako haijapotea ipo mahali salama, hali hii inarekebishwa.
 
Habari Samwel, pesa yako haijapotea ipo mahali salama, hali hii inarekebishwa.

Inarekebishwaje sasa??? maana nahangaika tangu jumamosi mbaya sana kila nikipiga simu kila anaepokea anasema lake na hamna cha maana nachopata jirekebisheni sana ila mnatutsha muamala wiki nzima haujafika uendako bora nikapange foleni.
 

Uki angalia hiyo attachment hapo hivyo ni vifurushi vya mwezi vyenye dakika na sms ambapo kwa tsh 19999 unapata dak 370 na 800 MB wakati 29999 ni dk 550 na 800 MB hapa dk hizo ni kupiga mitandao yote. Sina tatizo na hizo dakika za maongezi ila ni hivyo vifurushi vya Internet kwa bei hizo vipo chini sana kwa mwezi at least ingekuwa 2 GB basi ingekuwa nafuu. Mfano mimi kwa matumizi yangu Natumia kama 2 gb hivi sasa ina ni lazimu ninunue kifurushi cha 19999 ili nipate hizo dk 370 then ninunue unlimited internet bundle ya mwezi kwa sh 20000 ili nikidhi matumuzi yangu ya mwezi. Sasa kwa mwezi mmoja unatumia tsh 40000 kwenye simu just because vifurushi vyenu ni vidogo sana. Hii unatupa hasara. Yaani ni basi tu nilipo vodacom ndio ina speed nzuri Kinyume na hapo ningeshahama siku nyingi sana. Mi naomba mliangalie hilo at least kwenye ile package ya 19999 ya kupiga mitandao yote muweke bundle ya 2GB.
 

Attachments

  • 1416566261548.jpg
    45.9 KB · Views: 135
Vodacom naomba mnisaidie Salio langu linaisha bila kujua hatakama sijapiga sim mfano Jana nilikuwa na 4700 Leo sijaiona nimepiga customer care simu yangu haiunganishwi, what the hell happened?
 
Jamani Vodacom tuwekeeni 3G
Wilayani Ruangwa
Mkoani Lindi tumekua
Tunapata taabu sana katika kutumia huduma za internet
 
Vodacom naomba mnisaidie Salio langu linaisha bila kujua hatakama sijapiga sim mfano Jana nilikuwa na 4700 Leo sijaiona nimepiga customer care simu yangu haiunganishwi, what the hell happened?

Wanaiba, maswali mengine ni ya kijinga.
 
mimi ninatatizo na ufunguaji wa email kulingana na maelezo wanayonipa kwamba niandike neno VMAIL kwenda 15300 lakini kila nikituma wananiambia nijaribu tena sijui mtanisaidiaje kwa hilo ili kunifanya nifurahie zaidi kuwa katika mtandao wenu
natokea IRINGA
 
Mimi saiv Vida hata situmii kabisa,kwanza huduma zao ziko juuuu sana pia huduma ya internet iko slow sana siwapend saiv salio wanakat bila mpango
 
Vodacom nimenunua umeme siku ya NNE Leo sijapata token japo ni mdogo tu lakini ni hela yangu kila nikipiga customer care hawapokei
 
Hawa voda siku iz wanaboa sana yani kila siku wanapunguza MB kwenye Vifurushi vyao..mfano ukinunua cheka sh 500 vodacom kwenda voda com ulikuwa unapewa dakika 20 na MB 100.. sasa ivi ni MB 50 kwa dakika 19. sa sijui kwa nn wanafanya hivi hawa watu...hata taarifa hawatoi.. magumashi acheni basi ah.
 
Vodacom kuna tatizo aisee!ukiwejiunga na hivyo vifurushi namna vinavyokwisha kwa kweli ni balaa.Pili product ktk ofa zimekuwa km hazieleweki ipi ni nzuri kwa mteja.Mara Cheka bombastic,Mara Cheka zogo etc.Elimu itolewe hapo vizuri.Na pia kuna tatizo la kujiunga na hivyo vifurushi 'unajiunga muda huo huo kifurushi kimeisha ukisema ujiunge tena unaambiwa huwezi kujiunga sasa hapo ufanyeje na kifurushi kimekwisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…