Mara nyingi mtandao wa Vodacom umekuwa ukilalamikiwa na sisi wateja wenu lakini mmekuwa hamuelewi wala hamsikii kila siku ni kuibia wateja wenu,sasa tumechoka. Unakuta mtu unaweka salio katika simu yako na kuujinga na kifurushi chochote lakini muda mfupi unapotazama salio unakuta limekatwa na wakati bado kifurushi chako hakijaisha na unapopiga kitengo cha huduma kwa wateja,wahudumu wanakwambia uwapigie baada ya nusu saa au dakika fulani, hapo waweza kujiuliza hiyo namba ni ya binafsi au vipi ?
Kuweni makini na tabia hii kwani ipo siku na nyie mtajadiliwa bungeni na hapo ndo utakuwa mwisho wenu. Vodacom,mnauzi,mnakera na kutuibia mpaka basi. Acheni tabia hiyo,tushawachoka,ipo siku yatawakuta yalowakuta ESCROW,nyie jifanyeni hamna masikio.