Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mbona netwk kwa upande wa 3g zinasumbuaga area c dodoma? Unajiunga na vifurushi afu hutumii sababu ya mtandao... mnakera asee
 
Kiukweli tangia mmeniuzi kwa net zenu mbovu sasa nipo zantel kwenye 4G, naomba wateja msije nako huku mkajaa maana net yake yaukwehe
 
Voda kwenye hili swala la bundle mtatukimbiza wengi Cheka ya 500 kutoka mb 100 hadi mb 50 alafu mnasema tuunge cha 1000 kama tungekuwa mayo tusingelalamika 1000×30= 30000 yani mwezi mzima nitumie hela hili kwa CMU tuu hakuna mambo mengine. Alafu vifurushi vyenu vya unlimited in kharaa tu paka uwe na 1000 na kuendelea hebu angalieni AIRTEL na vifurushi vya OMG 400 mb 600, 600 mb 1024. Kwa usku sasa 1000 gb 30 kwa siku tatu huku nyie manatoa 1 gb acheni wizi jaribuni kutafalari upya juu ya bundle zenu na gharama maana mtapoteza Wateja
 
#Vodacom Tanzania# niambieni sababu ya msingi iliyowafanya kupunguza vifurushi vya cheka mb100 zikawa 50 dakika 20 zikawa 19 mmepunguza hata pale kwenye voda kwenda mitandao mingine lakni sms zinakuwa nyingi mno. Katika hayo yote mlioyafanya hamkutoa taarifa kwa wateja wenu kwanini? Ushauri wangu punguzeni sms ongeza kwenye dakika na mb kwakua asilimia kubwa ya watu matumizi yapo kwenye mb na dakika.
 
Mwenyekujua jinsi ya kuunganisha internet ya 3G ya Vodacom naomba msaada...natumia simu ya huawei ascends y330
 
Mara nyingi mtandao wa Vodacom umekuwa ukilalamikiwa na sisi wateja wenu lakini mmekuwa hamuelewi wala hamsikii kila siku ni kuibia wateja wenu,sasa tumechoka. Unakuta mtu unaweka salio katika simu yako na kuujinga na kifurushi chochote lakini muda mfupi unapotazama salio unakuta limekatwa na wakati bado kifurushi chako hakijaisha na unapopiga kitengo cha huduma kwa wateja,wahudumu wanakwambia uwapigie baada ya nusu saa au dakika fulani, hapo waweza kujiuliza hiyo namba ni ya binafsi au vipi ?

Kuweni makini na tabia hii kwani ipo siku na nyie mtajadiliwa bungeni na hapo ndo utakuwa mwisho wenu. Vodacom,mnauzi,mnakera na kutuibia mpaka basi. Acheni tabia hiyo,tushawachoka,ipo siku yatawakuta yalowakuta ESCROW,nyie jifanyeni hamna masikio.
 
Majizi haya... bundle zenu za kijinga... ndio nimeshahamia airtel na wengi watahama. bakini na bundle zenu za kiwizi
 
kwann uibiwe mkuu?km unaona unaibiwa c uhamie mtandao mwingine tu kuliko kupata presha.
 
Laini yangu ya voda naweka mara moja kwenye simu kwa mwezi kama kuishtua tu, siweki vocha. Ni kama ya dharura tu. Wameshaniibia sana hawa fisi maji. Mtandao ni AIRTEL.
 
Laini yangu ya voda naweka mara moja kwenye simu kwa mwezi kama kuishtua tu, siweki vocha. Ni kama ya dharura tu. Wameshaniibia sana hawa fisi maji. Mtandao ni AIRTEL.

Hii inatatanisha mi niko airtel, naona hawa ndo wadwanzi kabisa nilikuwa na mpango kuhamia voda.
 
kwann uibiwe mkuu?km unaona unaibiwa c uhamie mtandao mwingine tu kuliko kupata presha.
Ndio yaleyale mtu anaiba mnaishia kumtimua kazi badala ya kumshitaki.

Sawa atahama vipi pesa zake alizopoteza.?
 
Yan Mi hapa nataka nikipat nafas nkanunue na kujisajil airtel kwakweli..Voda mmeishiwa mbayA
 
kwa nini isiwepo university promoshen ya wiki nimechoka kuweka weka jero kila cku au marketing manager wenu hajajipanga majib tafadhari....
 
Hameni mtandao wandugu, kwani mnakomalia vodacom utadhani ndo mtandao pekee hapa nchini? Sio uongo hawa voda wamekua wapuuzi sana hasa kwenye vifurushi vya internet.
Msikubali kuteseka bila sababu kama tunavyoteseka kwa sababu ya kuitegemea Tanesco peke yake nchi nzima.
 
Voda mnazngua ni cku ya nne leo mfululizo nanunua vifurush ila kila nktuma sms haziend had nmeamua kununua line ya tgo il niweze kutuma sms,aisee jipangen coz mnafanya mabadlko ya huduma yanayo tuumiza watumiaj la cvyo uvumilvu utatushnda tutahama
 
Back
Top Bottom