Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

waheshimiwa vipi kuhusu Tigo Bundle ya 35 GB kwa waliojaribu
 
Mkuu location inahusika sana kwenye hili
Nikiwa golini Voda una weza kulia lakini nikiwa maskani ni balaaa, Tigo nikiwa golini inakimbiza mbaya nikifika maskani nikichefuchefu
 
Jamani Voda ni wezi aisee... Mie last saturday nilinunua muda wa maongezi kwenye mpesa. Ile nataka kujiunga na kifurushi nikaambiwa sina salio la kutosha wakati niliponunua salio walinipa confirmation ya kuwa salio limeongezeka.

Basi kwa vile nilikuwa ninahitaji mawasiliano ya haraka kwa wakati ule sikujali nikanunua tena salio na kujiunga.

Ila pesa yangu ndio ililiwa jamani, hivi tufanyeje ba huu wizi kwa kimachomacho??
Mie napata tatizo kama hilo na Airtel. Wkati mwingine nikitaka kununua kifurushi naambiwa sikufanikiwa nijaribu tena lakini wakati huo huo salio langu linaendelea kuliwa. Wataalamu tengenezeni petition ya online ambayo tunaweza kuisaini na kuipeleka TCRA, Wizara husika na Bungeni tukipinga wizi huu wa kampuni za simu.
 
Msije mkalogwa mkanunua bundle la mwezi kama nilivyofanya mimi. Nimenunua bundle la la Mwezi la gb 1. Nimetumia siku 3. Tena katika whats app. Baada ya siku 3 naambiwa eti eti zimebaki bundle 365mb. Leo asubuhi zimebaki bundle 46mb. Wezi wakubwa hawa vodacom. Msije kufanya makosa niliyofanya mimi i thought nina save kumbe ndo ninaibiwa. Nilikuwa naitetea sana inaposemwa vibaya hii kampuni. Kwa tukio hili sina imani nao tena. Wezi wakubwa.

Unatumia simu ya aina gani?
ume install applications zaidi ya moja?
zinakuletea notifications?

Kama una kubaliana na hayo niliyo kuuliza basi bundle lako linaweza kuisha na ukajikuta una laumu tuu, kama una apps zinakupa notifications ujue hapo pesa ina kuwa inatumika hivyo bundle linauwezo wa kuisha.

Vodacom-kazi ni kwako.
 
Unatumia simu ya aina gani?
ume install applications zaidi ya moja?
zinakuletea notifications?

Kama una kubaliana na hayo niliyo kuuliza basi bundle lako linaweza kuisha na ukajikuta una laumu tuu, kama una apps zinakupa notifications ujue hapo pesa ina kuwa inatumika hivyo bundle linauwezo wa kuisha.

Vodacom-kazi ni kwako.

My Lawyer, Kwa mimi binafsi natumia Nokia Tochi, sina huduma yoyote ambayo nimejiunga nayo. Sasa nashindwa kuelewa kwanini walinikata salio.
 
May be nyie Mimi fresh tu! Cheka bombastic ya mwezi kazi kazi tu.
 
My Lawyer, Kwa mimi binafsi natumia Nokia Tochi, sina huduma yoyote ambayo nimejiunga nayo. Sasa nashindwa kuelewa kwanini walinikata salio.

My boss,uliwasiliana na customer care 100? wewe tatizo lako ni tofauti na la mtoa mada.
Ulitakiwa uwapigie voda. Siku nyingine ukipata tatizo kama hilo watafute kupitia namba hii 15366 kabla ujajiunga na huduma nyingine.
 
My boss,uliwasiliana na customer care 100? wewe tatizo lako ni tofauti na la mtoa mada.
Ulitakiwa uwapigie voda. Siku nyingine ukipata tatizo kama hilo watafute kupitia namba hii 15366

Mkuu kiukweli sikuwapigia maana nilikuwa nina haraka na busy kwa siku hiyo, Halafu pia Customer Care kwa namba 100 inagoma kutoka kwa namba yangu mpaka nipige hiyo uliyotaja 15366 kwa gharama ya sh. 100. Na kama sina salio ndio siwezi kuwapata.
 
Binafsi nimewahi kutumia vodacom, tigo, airtel na zantel. Kote huko wana namna zao za kuiba ila vodacom kwa sasa inaongoza kukwapua pesa za wateja kinguvu tofauti na wengine wanaonyofoa kinyemela.

Tatizo kuu ni msimamizi wa mawasiliano ambaye ni TCRA, amewaacha wajanja watupige na tunapigika hasa bila hata msaada wowote.

Niliamua kuhama vodacom na niliahidi kuwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zangu wahame pia. Ninayo furaha kubwa kuwaambia kua ushawishi wangu umefanikiwa kwa 68% mpaka sasa toka December 2013.

Mwisho niwape pole wanaoendelea na vodacom maana ni chaguo lao kwa hiari yao. Japo huku niliko kwenye mitandao naibiwa pia lakini si kwa kasi kama ya voda. Wahudumu wa mitandao mingine wako makini na wepesi kusikiliza shida ya mteja. Jaribu huduma kwa wateja voda, oooh, kazi ni kwako.

mkuu niahamie mtandao gan?
 
Mm nimejiunga na kifurushi cha unlimited siku

Najuuuuuuta, nilijua kitakuwa n speed nzuri, spidi yake ni10-20kb/sec.
 
Jaman msije jiloga mkanunua vifurishi vya voda unlimited havina speed kabisa yani net inasinzia kabisa kweli vya bure gharama

nilichokifanya mimi,nimebomoa modem ya airtel ili iingie kila line,then natumia line ya voda.hiyo ndo atleast ina spid.airtel yenyewe ni bure kabisa.internet yenye spid huwa ni zantel.kwa hilo hawana mpinzani kati ya zile ambazo nilisha wahi kuzitumia.sema tu vigharama vyao viko juu kidogo.huwa nikiwa na mzigo mkubwa wa kupiga ndo huwae najipendelea zantel
 
Back
Top Bottom