Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari Mtoboasiri tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi, pole sana
Ndio kuhama gani huko?Kwwa nini kila siku wanapunguza bundle hawa vodacom....ngoja tuhamie vodacom.
ndicho kilichonitokea mm jana hadi choz lililenga...kwa kweli niliwamind sana hawa waduanzi...inawezekana wanaset vitu vyao...!!!?Vodocom wanaibiwa sana MPESA ila kwa kuogopa kuchafua jina lao wanakaa kimya na kuamua kulipiza kwa kuumiza wateja wao.
Hapo umenunua haiji, ikija ukijaribu kuunga kifurushi watakuambia mtandao unasumbua ili mradi tu pesa yako iliwe (ikiwa hujazima mobile data), badae wadakuambia huna salio la kutosha kujiunga na kifurushi.
Sasa kma kujiunga mtandao unasumbua, huo mtandao wakati pesa yako inaliwa taratibu unatoka wapi?
sasa sijui tutahamahama hadi lini hii mitandao??...na ukihamia mwingine karibisha mteja siku ya 1,2 3 wanakuumiza kama kawa!!Hawa wezi wamekuwa wakiniibia MB zangu mara nyingi tu. Nimehamia SMART.....so far so good!
Wamepokea maoni yetu na wameboresha kwa kiwango kikubwa at least wamekuwa wasikivu na wametenda
Hawa wezi wamekuwa wakiniibia MB zangu mara nyingi tu. Nimehamia SMART.....so far so good!
Habari Pampula jr tafadhali tunaomba namba ya simu PM kwa msaada zaidi.nisaidien voda wana nifirisi yaani jana nilikopa 900 leo nimelipa1000 deni lao lakini kila nikiweka vocha wanakata nimeweka hadi 4000 zote wanakata nikijaribu kukopa wanasema lipa mkopo wako wa awali kwanza nimechoka jamani na hawa wezi
Kujirekebisha ni pamoja na kuwarejeshea wale waliowaibia
Mkuu hawa jamaa nishawahama mwaka huu, line yangu ya Voda ilikuwa na tatizo la kutopiga simu ila kupokea simu pamoja na kuandika sms na kutumia net ilikuwa poa, nilihangaika na customer care mpaka nikakata tamaa, siku nikaamua kuwaibukia pale mlimani city, nikawaambia tatizo, mwisho wa siku eti wananiambia niformat simu ndo ina tatizo, sasa nikawa najiuliza kama simu ndo tatizo mbona line za mitandao mingine zinafanya kazi vizuri, kuanzia hapo nikawatema, jana tu dada yangu alikuwa analalamika anasalio la kutosha lakini kila akijaribu kuunga kifurushi anaambiwa hana salio la kutosha
Habari tzbiz pole sana kwa suala hili na tunaomba kufafanua namna Happy Hour inavyokuwa. Ni kwamba huduma hii inakupa dakika 60 kupiga simu kuanzia muda uliojiunga, hii inaamanisha kuwa ukijiunga saa 2 asubuhi huduma yako itakwisha dakika 60 kutoka saa 2 asubuhi kwa maana ya saa 3. Ukipiga simu saa 2 dk 40 unakuwa umebakiza dakika 20 kufikia mwisho wa kifurushi chako.
Kwahiyo kifurushi ulichojiunga saa 1:30 cha dakika 20 ilikuwa ni sahihi kupokea ujumbe kuwa kifurushi chako kimekwisha dakika 30 baada ya kujiunga.Tunaimani maelezo haya yamefafanua vyema suala hili
Tumia Zantel ndio baba lao, hata km hujajiunga unapiga mitandao yotee bila shida
haya nilikuwa nje ya mtandao. nimerudi, nimesoma maelezo, na nimekuelewa. Kwa nini msibadili mtindo kuleta thamani ya fedha ya watumiaji wa mtandao wenu? huoni kama huo mtego wa kusema dakika 60 unadangaya watu kwa kuwa hakuna kipengele cha kusema LAZIMA UANZIE MWANZONI MWA HIYO SAA?
Kwanini msiweke hiko kipengele kuokoa watu wanaojiamulia kununua hiyo happy hour bila kuangalia kama wamenunu dakika ngapi ndani ya muda?
Wewe Vodacom tanzania hapo bado haujakwepa lawama ya udanganyifu hata kidogo.... Hiyo katika marketing inaitwa Deceptive Advertising, na ni jinai ya kibiashara hivyo. Badilikeni!
Nadhani mnajua kuwa huu ni mtandao wenye watu wengi tanzania kwa hiyo wanajua advantage yao sokoni. Kila mtu anaelewa ukisema uwingi kwa watz inaimply kwn v2 vikuu vitatu. 1. ignorance 2. non educated 3. njaa. Popote penye watz kwa wingi ujue v2 hivyo vipohaya nilikuwa nje ya mtandao. nimerudi, nimesoma maelezo, na nimekuelewa. Kwa nini msibadili mtindo kuleta thamani ya fedha ya watumiaji wa mtandao wenu? huoni kama huo mtego wa kusema dakika 60 unadangaya watu kwa kuwa hakuna kipengele cha kusema LAZIMA UANZIE MWANZONI MWA HIYO SAA?
Kwanini msiweke hiko kipengele kuokoa watu wanaojiamulia kununua hiyo happy hour bila kuangalia kama wamenunu dakika ngapi ndani ya muda?
Wewe Vodacom tanzania hapo bado haujakwepa lawama ya udanganyifu hata kidogo.... Hiyo katika marketing inaitwa Deceptive Advertising, na ni jinai ya kibiashara hivyo. Badilikeni!