Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mkuu hongera kwa uvumilivu, wengine tulishahama kitambo sana baada ya kujibiwa kwa kebehi na jeuri kwenye hizo wanaita huduma kwa wateja. Niko huru kwa sasa.
 
Bora umeliona hilo Hawaii jamaa wanna gharama kubwa kuliko mtandao wowote,hawana lolote hao

wanaboa sana.. ila nadhani ni utekelezaji wa slogan yao ya KAZI NI KWAKO..kuondoka au kubaki.
 
Mkuu hongera kwa uvumilivu, wengine tulishahama kitambo sana baada ya kujibiwa kwa kebehi na jeuri kwenye hizo wanaita huduma kwa wateja. Niko huru kwa sasa.

dahh.. wanaboa sana mkuu.. bt inafika mahali uvumilivu mtu unamshinda..
 
Usipoanza wewe nawahama yaani hawajifunzi kwa tigo...airtel na zantel...wamekalia kusema mitaani nafanya kazi voda na kula pesa za wizi tu kutoka kwa wateja wao...

Kuna mmoja alitoa wazo kwenye page yao ya facebook kwamba kwenye menu yao ya *149*01# waweke muamala wa kurudi nyuma kama mteja kagundua kakosea wateja wanazidi kutoa maoni wao wamekaa kimya nina ndugu zangu wawili wamehamia tigo na airtel..mda si mreu nawafuata nyie wadai.Voda nimechoka nao nimechoka nimechokaaa
 
nimekuwa mteja wako kwa muda mrefu sana lakini sasa naona ni muda mwafaka kukuhama..

mimi ni mtanzania ambae ninataka mtandao wenye garama nafuu za mawasiliano..

lakini hata kama nimekuwa mteja wako hujanifunga kiasi cha kuendelea kuung'ang'ania wakati naona kuna uhuru kwingineko..

1.siku hizi kupiga simu voda huduma kwa wateja UNALIPIA.. UJINGA HUU.. mbaya zaidi wahudumu wanabaki kukupiga bla blaaa na kukata simu bila kupata huduma inavyostahili na ukirudia kupiga unalipia tena na tenaaa..

2. Huduma ya m-pesa imebaki kuwa juu kuliko mtandao mwingine hapa tz kama airtel money na tigo pesa.

3. huduma za cheka bombastick zimepanda bei hasa ya kupiga mitandao mingine.. MNAKAZANA KULETA HUDUMA ZISIZO NA MASHIKO KAMA CHEKA ZOGO YA KUPIGA VODA KWENDA VODA. hupati sms wala mb za internet ukiwa na cheka zogo.. huu ni usen........ na mtapigwa bao huku mkijifanya mtandao unaoongoza tz
mitandao mingine kama airtel wameleta hadi vocha za extreem tu mfano sh 500 unapata dk 15 mitandao yote MB na sms kibao.. NITAWAACHA

CHA KUFANYA HAPA NI KUBORESHA HUDUMA VINGINEVYO KAZI ITAKUWA KWANGU KUONDOKA KWENDA KWENYE MITANDAO YENYE HUDUMA NAFUU..

Duh, First Born ushauri wako umechelewa kuwafikia. Mimi nimeachana nao rasmi jana, tarehe 31 July. Wana mayai viza kbao. Umesahau na lingine. Wanauza/vujisha mawasiliano ya wateja, hawana siri, hawana maadili. Ngoja wenye akili tuondoke, mmoja mmoja!!
 
dahh.. wanaboa sana mkuu.. bt inafika mahali uvumilivu mtu unamshinda..

Mimi walikula fedha yangu halali ya Tanzania ya shilingi elfu tano kimaajabu ajabu, nikawapigia huduma kwa wateja kwa ile namba yao ya kulipia, majibu yao eti niwapigie baada ya saa 24, nikafanya hivyo lakini majibu yaleyale. Sikuona tabu kukavunjilia mbali ka kadi kao na kukubali kula hasara ya kiasi hicho. Sasa hakuna msongo tena, ni uhuru wa kujiachia utakavyo.
 
Usipoanza wewe nawahama yaani hawajifunzi kwa tigo...airtel na zantel...wamekalia kusema mitaani nafanya kazi voda na kula pesa za wizi tu kutoka kwa wateja wao...

Kuna mmoja alitoa wazo kwenye page yao ya facebook kwamba kwenye menu yao ya *149*01# waweke muamala wa kurudi nyuma kama mteja kagundua kakosea wateja wanazidi kutoa maoni wao wamekaa kimya nina ndugu zangu wawili wamehamia tigo na airtel..mda si mreu nawafuata nyie wadai.Voda nimechoka nao nimechoka nimechokaaa

hapa ni kununua kisimu cha kichina.. line yao nitaiweka hewani ili tu wale wasioifahamu namba yangu mpya wasinikose hewani.. bt kupiga simu, vocha na huduma zingine nitazifanya kwa line mpya ya mtandao mwingine...
 
Mimi walikula fedha yangu halali ya Tanzania ya shilingi elfu tano kimaajabu ajabu, nikawapigia huduma kwa wateja kwa ile namba yao ya kulipia, majibu yao eti niwapigie baada ya saa 24, nikafanya hivyo lakini majibu yaleyale. Sikuona tabu kukavunjilia mbali ka kadi kao na kukubali kula hasara ya kiasi hicho. Sasa hakuna msongo tena, ni uhuru wa kujiachia utakavyo.

nakuja mkuu.. niko njiani.. nimeshaweka mikakati ya kutosha ambayo hayataniathiri nitakapohamia kwingine dhidi ya marafiki zangu.
 
nakuja mkuu.. niko njiani.. nimeshaweka mikakati ya kutosha ambayo hayataniathiri nitakapohamia kwingine dhidi ya marafiki zangu.

Karibu sana mitandao yenye nidhamu kwa wateja, huko voda ni majanga matupu.
 
Yani hawa jamaa vifurushi vya 1000 wao wanakata 1000 na mia..!
 
Mie line yangu voda iko hewani lakini inaenda mwezi sijaweka vocha ni mwendo wa kupokea simu tuk kama simu ya mezani!
 
mimi kila nikinunua luku naipata bada ya masaa na siku nyingine ndo nitolee. imenibid lain ibaki ya kupigiwa tu na siku mojamoja kubrowse. na ukitaka amin kuwa ndo wanapotea hata comissio zao kwa watu wa mpsea zinazidi pungua karibia watafunga tu.toka lin kuch kuch hotahe akamzidi kaborou
 
niliwahi kusikia tetesi kua kuna viongozi wa twawala wana hisa humo voda sasa isije ikawa wanatimiza ilani yao maana nimeliwa nilikopa 900 sasa wakati wa kulipa ikawa kila nikiweka vocha ya buku inakatwa hadi ikafika 5000 wanakula tu nilipowapigia wakazingua sina hamu
 
Mie line yangu voda iko hewani lakini inaenda mwezi sijaweka vocha ni mwendo wa kupokea simu tuk kama simu ya mezani!

ndo mkakati nilionao.. nitakanunua kasimu ka elfu 15 ambacho kazi yake ni kupokea tu wale ambao hawaijui namba mpya..
 
Ni kweli kazi ni kwako...! Kubaki au kuondoka! Mm ni mteja wao wa miaka mingi sana tangia vodacom inaingia nchini ila kwa sasa nimewahama hasa jwebye data receiving natumia sana mtandao wa tigo au Airtel ni nafuu na sio wezi km vodacom...vodacom ni wezu balaa! Wanakuibia mteja mchana kweupeee...hawafai hawa jamaa.mkuu hama mapema watakufilisi hawa...
 
Hivi hapa wangekuwa na uwezo, wanatamani kama wampe BAN kila anayeandika hapa ila sema tu hawana meno, huku ni kuchanana tu.
Mimi kuna siku nilijaribu kuwachana kidogo tu kuhusu huduma zao, duh! kwa hasira wakaamua kuni-block kabisa kupitia facebook.
 
Back
Top Bottom